Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakiendelea na kikao cha baraza ndani ya ukumbi wa halmashauri.
.......... HABARI KAMILI............
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto wameaswa kuwasimamia watendaji wa kata na vijiji katika maeneo yao ili kumaliza migogoro. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa wakati akitoa maelekezo ya serikali katika kikao cha baraza la madiwani , kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri , mwishoni mwa mwezi Juni 2018.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Magessa amesema “ Nawashukuru sana madiwani mnaendelea kusimamia amani katika maeneo yenu. Sasa tunaelekea mahali Fulani ambapo pana matumaini. Kila kijiji mtakachopita waulizeni watendaji daftari lao la migogoro liko wapi?Mkiendelea kuwasimamia hao migogoro itakwisha.Katika uchunguzi wetu tumebaini kwamba kule chini watendaji wa kata na vijiji walifika mahali wakaacha kushugulikia migogoro, kwa hiyo akabakia diwani, DED,DC,RAS na mawaziri .Ndio wanaoshughulikia migogoro ya vijiji,sasa matokeo yake yalikuwa magumu kidogo”
Aidha Mhe. Magessa amesema kwamba kama waheshimiwa madiwani wataendelea kuwasimamia watendaji kufanya kazi zao,migogoro iliyobaki wataendelea kuimaliza.
Wilaya ya Kiteto imekuwa ikikumbwa na migogoro mingi ya ardhi, ambapo viongozi wa vijiji,kata, wilaya ,mkoa na hata taifa wameendelea kushughulika kumaliza migogoro hiyo. Hadi sasa iko katika hatua nzuri, hali ya amani na utulivu imerejea kwa kiasi kikubwa ndani ya wilaya hiyo.
.......... MWISHO..........
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa