Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel akizungumza wakati akifunga kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya halmashauri kwa mwaka 2019/2020.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel akiongoza kikao .
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto akitoa ufafanuzi kuhusiana na michango ya Wahe. Madiwani kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kiteto Ndg. Mohamed Kiondo akizungumza wakati wa kikao .
Wahe. madiwani wakichangia kuhusiana na bajeti iliyowasilishwa .
Wahe. madiwani wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa bajeti.Aliyesimama mbele (mwenye joho Jeusi ) ni kaimu Afisa mipango (W) ambaye ndiye aliyewasilisha bajeti hiyo Ndg. Edga Kavenuke.
Wataalamu kutoka idara mbalimbali za halmashauri ya wilaya ya Kiteto wakiwa kikaoni.
........HABARI KAMILI.........
Madiwani Watakiwa Kushiriki Katika Ukusanyaji wa Mapato
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mheshimiwa Lairumbe Mollel amewataka waheshimiwa madiwani kushirikiana na wataalamu wa halmashauri katika ukusanyaji wa mapato,ili bajeti waliyoipitisha iweze kutekelezeka.Mhe. Lairumbe ameyasema hayo wakati wa kikao cha kupitisha bajeti ya halmashauri kwa mwaka 2019/2020.
Akizungumza wakati akifunga kikao hicho Mhe. Mollel amesema kwamba fedha zilizopitishwa kwenye bajeti ziko kwenye makaratasi,ili zipatikane ni lazima ushirikiano uwepo.Akisisitiza kuhusu ushirikiano huo, Mhe Mollel amesema “Bajeti ni mapendekezo tu, uhalisia wake unatokana na ukusanyaji wa mapato.Ukusanyaji wa mapato ndio utatupa dira kwamba halmashauri yetu itaendaje.Sisi kama madiwani kule kwenye kata zetu, tuhakikishe kwamba tunapamba kudhibiti utoroshwaji wa mazao.Na tunasimamia vizuri ukusanyaji mapato.Usimamizi wa mapato sio wa Mkurugenzi ,wala sio wa wataalam pekee,kazi hiyo ni ya kwetu sisi zaidi kama wasimamizi wa halmashauri hii”.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kiteto ndugu Mohamed Kiondo ametilia mkazo kauli ya mwenyekiti wa halmashauri ambapo amewataka waheshimiwa Madiwani kusaidia usimamizi ukusanyaji mapato kwenye kata zao,ili miradi inayokusudiwa kutekelezwa kupitia bajeti hiyo iweze kutekelezeka.
Aidha ndugu Kiondo ameipongeza halmashauri kupitia mkurugenzi mtendaji wake ndugu Tamim H. Kambona kwa miradi yenye viwango, ambapo amesema kwamba wilaya ya Kiteto ndiyo inayoongoza mkoani Manyara kwa miradi yenye viwango.
Katika hatua nyingine diwani wa kata ya Kaloleni Mhe. Christopher Permeti amempongeza Mkurugenzi mtendaji pamoja na wataalam wa halmashauri kwa kuzingatia mapendekezo ya kamati katika bajeti hiyo ambapo amesema kwamba mapendekezo yote waliyoyatoa kwenye vikao vya kamati yamefanyiwa kazi.
Kikao hicho cha baraza la madiwani ambacho ajenda yake kuu ilikuwa ni kupitisha bajeti, kilitanguliwa na vikao vya kamati za kudumu za halmashauri ambapo kamati zote zilipitia na kujadili kwa kina na kutoa mapendekezo yake kuhusiana na bajeti hiyo. Kikao kilihitimishwa baada ya Wahe. madiwani wote kwa kauli moja kuridhia na kupitisha bajeti ya sh. 31,707,464,722.75, ambapo kati ya fedha hizo sh. 2,273,486,000/= zinatarajiwa kupatikana kupitia makusanyo kutoka katika vyanzo ya ndani ya Halmashauri.
.
........MWISHO.........
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa