Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, iliendesha mafunzo kwa viongozi wapya wa Serikali za Mitaa walioteuliwa katika uchaguzi wa tarehe 27 Novemba 2024. Mafunzo hayo yaliyohusisha Wenyeviti wa Vijiji 63, Wenyeviti wa Vitongoji 278, Wajumbe Mchanganyiko 754 na Wajumbe Wanawake 504, yalifanyika kwa kugawanya washiriki katika kanda tatu kulingana na tarafa zao Desemba 16-18,2024.
Lengo la mafunzo lilikuwa kuwaongezea uwezo wa kusimamia na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Mafunzo yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, ambaye aliwapongeza viongozi hao kwa kuchaguliwa na kuwasihi kusimamia haki, maendeleo, mipango ya ardhi, na usalama wa wananchi huku wakikataa rushwa.
Mada zilizofundishwa zilihusu sheria, uongozi bora, usimamizi wa fedha, mipango ya maendeleo, na udhibiti wa ardhi. Viongozi walitoa ahadi ya kusimamia haki na kuhakikisha miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati. Mafunzo haya yameongeza uelewa wao na kuimarisha uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa manufaa ya wananchi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa