Viongozi wa Kamati ya Dini Mbalimbali Wilayani Kiteto, wakiongozwa na Mch. David Kalinga, Afisa Programu wa Mahusiano ya Dini Mbalimbali kutoka CCT, Desemba 18, 2024 wamekutana na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema, pamoja na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Akizungumza katika kikao hicho kifupi, Mhe. Remidius Mwema amewashukuru viongozi hao kwa ushirikiano wao mzuri na serikali katika kufanikisha kazi mbalimbali za maendeleo wilayani Kiteto. Aidha, amewapongeza kwa jitihada zao katika kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27,2024..
Mhe. Mwema pia alitoa wito kwa viongozi hao wa dini mbalimbali kuendelea kulinda na kudumisha amani katika jamii, pamoja na kuliombea taifa kwa ujumla.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa