Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi, Bi. Elizabeth Mlaponi, akiwa ameambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, wamefanya ziara ya ufuatiliaji wa maendeleo ya miradi ya BOOST inayotekelezwa kupitia divisheni hiyo.
Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa jumla ya vyumba vya madarasa 21 na matundu ya vyoo 48 katika shule za msingi saba.
Jumla ya thamani ya miradi hii ni zaidi ya shilingi milioni 780.
Shule zinazotekelezewa miradi hiyo ni:
1. Shule ya Msingi Enguserosidan (vyumba vya madarasa 2, matundu ya choo 6).
2. Shule ya Msingi Nalangtomon (vyumba vya madarasa 2, matundu ya choo 6).
3. Shule ya Msingi Olgira
(vyumba vya madarasa 2, matundu ya choo 6).
4. Shule ya Msingi Malimogo (vyumba vya madarasa 2, matundu ya choo 6)
5. Shule ya Msingi Kurash (vyumba vya madarasa 3, matundu ya choo 6).
6. Shule ya Msingi Olkitikiti (vyumba vya madarasa 3, matundu ya choo 6)
7. Shule ya Msingi Oloimugi (vyumba vya madarasa 7, matundu ya choo 12)
Ukaguzi huu una lengo la kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora unaostahili, kwa wakati, na inakidhi mahitaji ya wanafunzi katika maeneo husika.
Bi. Mlaponi amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu hii muhimu, huku akisisitiza uwajibikaji na matumizi bora ya fedha za miradi kwa manufaa na maendeleo ya wilaya ya Kiteto.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa