• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Madiwani Kusimamia Upandaji Miti Kiteto

Imetumwa : March 29th, 2018

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akitoa maelekezo kuhusu namna ya kutekeleza zoezi la upandaji miti.Katika uzinduzi wa zoezi hilo uliofanyika  katika  eneo la mlima simu - kijiji cha Njoro, wilayani Kiteto.


Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akipanda mti  kama ishara ya kuzindua  zoezi la upandaji miti .Tukio hili limefanyika  katika  eneo la mlima simu, kijiji cha Njoro wilayani Kiteto.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akiunyweshea maji mti alioupanda ,katika uzinduzi  wa zoezi la upandaji miti  uliofanyika  katika  eneo la mlima simu, kijiji cha Njoro wilayani Kiteto.


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel  akipanda mti katika uzinduzi wa  zoezi la upandaji miti uliofanyika katika  eneo la mlima simu, kijiji cha Njoro wilayani Kiteto.


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona ( aliyevaa tisheti nyeupe yenye mistari ), waheshimiwa madiwani pamoja na watumishi wakiwa ndani ya basi lililowasafirisha kwenda katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti  uliofanyika katika eneo la mlima simu- kijiji cha Njoro, wilayani Kiteto.

Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto  baada ya kumaliza  kupanda miti katika uzinduzi wa  zoezi la upandaji miti  uliofanyika  katika  eneo la mlima simu, kijiji cha Njoro wilayani Kiteto.


Basi la Kampuni ya Struggle investment lililowasafirisha watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwenda katika uzinduzi wa zoezi la upandaji miti uliofanyika katika eneo la mlima simu - kijiji cha Njoro  wilayani Kiteto.



..........HABARI KAMILI..........



Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Magessa amewataka waheshimiwa madiwani kusimamia zoezi  la upandaji miti katika kata zao.Mhe. Magessa ametoa agizo hilo baada ya kuzindua  zoezi la  upandaji miti  ,uzinduzi  ambao  umefanyika katika  eneo la mlima  wenye   minara ya simu maarufu kama  mlima simu - kijiji cha Njoro , kata ya Njoro wilayani Kiteto  mapema leo.


Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Mhe. Magessa amesema kwamba zoezi hilo la upandaji miti ni la kitaifa na kwamba kila wilaya inatakiwa kupanda miti isiyopungua 1,500,000.katika kuhakikisha kwamba zoezi hilo linatekelezwa Mhe. Magessa  ametoa maelekezo ya namna ambavyo kazi hiyo itafanyika .Haya hapa ni maelekezo ya Mhe. Magessa ‘‘Tunatakiwa kupanda miche 1,500,000 katika wilaya yetu. Tumeitana hapa sio  kwa sababu ya kuonyesha kwamba tunapanda nini leo,shida yetu kubwa ni kuanza kupanda miti leo.Katika eneo hili leo tutapanda miti 500,baada ya kumaliza hapa , zoezi hili linahamia kwenye kata. Tuna kata 23, kila kata itapanda miti 500. Kila diwani aliye hapa  anakwenda kwenye kata yake kuhakikisha kwamba idadi ya miti aliyoambiwa kupanda  anaipanda kwenye kata yake.Hili lifanyike kabla  ya kuisha mwezi  wa 4”.


Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel amesema kwamba  zoezi hilo liwe endelevu  kwa wananchi wa Kiteto,wapande miti kweye maeneo yao yote, maeneo ya taasisi pamoja na makazi yao ili kurudisha uoto wa asili.Akizungumzia madhara yaliyosababishwa na ukataji miti ovyo ambao ulikuwa ukifanyika siku za nyuma, Mhe Mollel amesema “tulifika mahali hali ilikuwa mbaya, hata mabadiliko ya tabia nchi yamesababishwa na ukataji miti.Lakini naamini wananchi wa Kiteto wamejifunza, wamejua madhara ya ukataji miti, na umuhimu wa kupanda miti.Wito wangu kwao ni kwamba tupande miti, tutunze mazingira ili tuweze kurudisha hali ya Kiteto kama ilivyokuwa zamani”.


Kadhalika mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamimu Kambona amesema kwamba zoezi hilo la upandaji miti ni  la kitaifa,na wao kama halmashauri wamekwenda na watumishi katika uzinduzi wa zoezi hilo  kwani watumishi ndio kioo cha jamii. Na kwamba watu wengi ambao sio  watumishi wa serikali wanaangalia watumishi wanafanya nini ndipo na wao wafanye. Hivyo kitendo  cha  watumishi kushiriki katika uzinduzi huo kitawapa hamasa wananchi kujitokeza kwa wingi katika utekelezaji wa zoezi hilo. Aidha ndugu Kambona ameutaka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kulipa deni inalodaiwa na halmashauri ya wilaya ya Kiteto kiasi cha shilingi 42,000,000 (milioni arobaini na mbili)  ili fedha hizo zitumike katika uendelezaji  wa zoezi la kupanda miti wilayani Kiteto.


Zoezi hilo la upandaji miti litaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali wilayani Kiteto ndani ya mwezi April ,na linatarajiwa kurudiwa tena mwezi Julai 2018.



..........HABARI KAMILI..........

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa