Katika kuhakikisha kuwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto wanajaza kwa ufanisi majukumu yao katika Mfumo wa Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma (e-utendaji), Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imeendesha mafunzo mengine kuhusu mfumo huo wilaya hapa.
Mafunzo haya ambayo yamefanyika Juni 12,2025 yalifunguliwa na Katibu Tawala wa Wilaya, Ndg. Mufandii Msaghaa, yalilenga kuwajengea watumishi ufanisi katika uandaaji wa mpango kazi na ujazaji wa utekelezaji wa mpango huo katika mfumo huo.
Katika mafunzo hayo, wakufunzi walielezea makosa mbalimbali ambayo watumishi huyafanya wakati wa uandaaji wa mpango kazi na kueleza njia za kuepuka makosa hayo.
Aidha watumishi walipewa fursa ya kuuliza maswali mbalimbali kuhusu changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa wanatumia mfumo huo.
Vilevile wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wasimamizi wa vituo walipewa mafunzo ya jinsi yakuwafanyia tathmini watumishi na kuwasisitiza kufanya hivyo ili kuwawezesha watumishi kupanda daraja kwa wakati uliokusudiwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa