Afisa Mwandikishaji Ngazi ya Jimbo Bw. Tamim H. Kambona ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Akifungua Mafunzo Hayo.
Mh. Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto Johakimu J. Mwakyolo Akisalimia na Kuanza Zoezi la Kuwaapisha Watendaji Wote wa Wilaya ya Kiteto
Hapo juu ni washiriki wenyewe wa zoezi hili wakinawa mikono kabla hajaingia ukumbini hapo.
Washiriki wa mafunzo haya kama wanavyoonekana mpenzi msomaji
------------------------------------------------------------ HABARI KAMILI ------------------------------------------------------------
Katika mafunzo hayo mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw.Tamim H. Kambona alisisitiza washiriki wote kuwa na tahadhari ya ugonjwa wa Corona "Covid 19" kwa kufuata kanuni za kitabibu zinazotolewa na Serikali. hata hivyo Bw. Kambona aliongeza kuwa kila mtu awe makini kwa kusikiliza na kufanya mazoezi kwa vitendo kwa wingi ili kila mmoja akielewa vizuri itaongeza ufanisi wa uboreshaji wa daftari hili katika Halmashauri yetu.
Mafunzo haya ni ya siku moja tu, ambapo kesho kutwa tarehe 17.04.2020 tutaanza uboreshaji wa daftari hili kwa muda wa siku tatu hadi tarehe 19.04.2020 katika Kata zote 23 za Wilaya yetu ya Kiteto ambapo kila kata itakuwa na kituo kimoja chenye Mashine ya kuandikishia (BVR Kit) moja kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12 jioni.
Kwa kuzingatia hali ya kukabiliana na ugonjwa wa Corona "Covid 19" kanuni zote za kiafya zilifuatwa katika hatua zote kwa kuwepo ndoo yenye maji safi yanayotiririka ya kunawia na vitakasio vya aina mbalimbali ambapo kila mtu anayeingia na kutoka lazima apitie hatua hizo, katika ukaaji pia zingatio la mita 1 hadi 2 ulizingatiwa ipasavyo na muhimu zaidi walitumia muda mchache kufanikisha haya ili kujikinga na ueneaji wa ugonjwa huu wa Corona "Covid 19".
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji imetoa matangazo ya kutosha kwa njia ya kubandika matangazo hayo kwenye mbao za matangazo Ofisi zote za Vijiji na Kata na maeneo mengine maarufu pia kutangaza kwa kutumia magari kwa Wilaya nzima katika kata zote kuhamasisha wananchi kufika vituo husika kuhakiki taarifa zao kwa muda na tarehe tajwa hapo juu ili kuweza kurekebisha taarifa zao kwa wale wenye mahitaji.
Pia unaweza kuhakiki taarifa zako kwa njia ya mtandao kupitia simu yoyote ya mkononi kwa namba *152*00# kisha fuata maelekezo utakayokuwa unapewa lakini waweza ingia kwenye tovuti ya tume ya uchaguzi yenyewe kwa anwani ya www.nec.go.tz inashauriwa pia ni vema mtu akatumia njia hii kuhakiki taarifa zao kupunguza mzunguko wa muhusiaka na kuweza kuzuia janga la Corona "Covid 19"
Katika zoezi hili suala la kuzingatia kanuni za kuzuia ueneaji wa Corona "Covid 19" utaendelea kwa kila kituo kuwepo kwa ndoo mbili moja ya maji ya kunawia na nyingine kukingia maji machafu ikiwemo na kitakasa mikono, pia kwa kila foleni itakayokuwepo basi umbali husika utazingatiwa.
Mwisho kila muhusika azingatie maelekezo yote atakayopewa na akafanye kazi kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu ili ufanisi uwe kwa asilimia mia moja.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa