Wataalamu Mbalimbali Wakitekeleza Majukumu Yao ya Kuandikisha Wananchi Kisha Kusajiri SIM-CARD zao Hapo Hapo Sehemu ya Chini ya Mti Mjini Kibaya Kama Inavyoonekana kwenye Picha Hapo Juu.
--------------------------------------------- HABARI KAMILI ---------------------------------------------
Zoezi la Usajiri wa "LINE" za simu "Subscriber Identification Module CARD - SIM CARD" ni zoezi la kitaifa lililoanza mwezi mei 2019 na litaisha tarehe 31.12.2019 ambapo kwa mtu ambaye hatasajiri kwa muda tajwa hapo juu basi hataweza kutumia sim - card hiyo tena.
Kama ilivyotajwa hapo juu zoezi hili ni la muda maalumu lakini uhamasishaji huu na uandikishaji huu ni kwa kuwafata wananchi katika vituo vya hadhara kama hiki cha kibaya mjini, ni kwa siku tatu tu kuanzia leo tarehe 31.10.2019 hadi kesho kutwa tarehe 02.11.2019 kwa mujibu wa Bw. Ombeni Mbesele ambaye ni Afisa wa NIDA wa Wilaya ya Kiteto. Baada ya hapa zoezi hili litaendelea katika vituo vya awali kama kawaida, walengwa wa zoezi hili ni wamiliki wote wa "line" za simu Tanzania wanatakiwa kusajiri "line" zao kwa mujibu wa agizo la serikali kwa mfumo mpana zaidi unaohusisha matumizi ya vidole vya muhusika katika kuweka kumbukumbu za mtumiaji. Lengo kuu la Serikali ni kuwasaidia wananchi katika masuala mbalimbali ya kiusalama ili kuleta maendeleo yenye tija yanayosukumwa na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya simu nchini.
Hadi sasa wananchi wengi hutumia simu katika mawasiliano ya sauti, kutumia picha za video na mnato kwa kutumia mitandao ya kijamii pia kutumia pesa mtandao katika kukamilisha miamala mbalimbali kama vile kununua vifurushi vya simu, kununua LUKU, ankara za maji, ving'amuzi, manunuzi ya bidhaa mbalimbali, faini za barabarani, malipo ya Serikali kama vile elimu, ardhi, TRA na zingine nyingi yote haya ni mapinduzi makubwa sana katika tasnia nzima ya mawasiliano yanayopelekea uchumi kukua kutokana na kuongezeka kwa mzunguko wa kifedha mtandaoni kiurahisi muda wowote na popote, ambapo ongezeko kubwa la ajira za kutosha kwa wananchi nchi nzima limeonekana.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya kiteto wamehimizwa kuendelea kusajiri "line" zao kuepuka usumbufu utakaojitokeza baada ya muda wa zoezi hili kuisha.
Hata hivyo wakieleza kwa muda tofauti tofauti wananchi wamefurahishwa na wameishukuru serikali kwa kuwa sikivu kwa kuwafuata maeneo waliyopo ili kukamilisha zoezi hili nyeti.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa