• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Miradi Yenye Viwango Yaipaisha Wilaya ya Kiteto

Imetumwa : September 27th, 2018

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho akipokea taarifa ya ujenzi wa bweni la wavulana ( Mhe. John P.J Magufuli) lililojengwa  katika shule ya sekondari ya Engusero.Mara baada ya kusomewa  taarifa hiyo kabla ya ufunguzi wa bweni hilo.

Kiongozi wa mbio za mwenge Ndg. Charles Francis Kabeho akikagua vitanda vilivyopo ndani ya bweni la Mhe. John P.J Magufuli  katika shule ya sekondari Engusero kabla ya kufungua bweni hilo, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru wilayani Kiteto.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho akikata utepe kama ishara ya kufungua  bweni la Mhe. John P.J Magufuli  katika shule ya sekondari Engusero wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru Kitaifa Ndg. Charles Francis Kabeho akipanda mti, kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa utunzaji mazingira. Zoezi  hilo la upandaji miti limefanyika katika shule ya sekondari Engusero wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho  akijiridhisha kuhusu vipimo halisi vya barabara, kabla ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Namelock - Sunya .Tukio hili limefanyika  Namelock wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho akizindua mradi wa maji katika mtaa wa Ngarenaro.Tukio hilo limefanyika wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge  wa Uhuru Kitaifa 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho akimtwika ndoo ya maji mmoja kati ya wanawake wa mtaa wa Ngarenaro kama ishara ya ufunguzi wa mradi wa maji, uliojengwa katika mtaa huo. Tukio hilo limefanyika  Ngarenaro wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Kiteto.




................HABARI KAMILI...........



Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ndugu  Charles Francis Kabeho ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa miradi ya maendeleo yenye viwango. Kabeho ametoa pongezi hizo wakati akifungua mradi wa bweni la wavulana katika shule ya sekondari Engusero lijulikanalo kama Mhe. John P.J. Magufuli .


Kabeho ametoa pongezi kwa Mkuu wa wilaya, Mwenyekiti wa halmashauri,Madiwani,Mkurugenzi mtendaji, wakuu wa idara ,pamoja na watumishi wote wa halmashauri  ya wilaya ya Kiteto kwa usimamizi mzuri wa miradi pamoja  na kujituma ambako kumesababisha kujengwa kwa bweni zuri, na kwa gharama ndogo.


Akisisitiza kuhusu pongezi hizo Kabeho amesema “ Kwanza niwapongeze Kiteto kwa jengo zuri, sambamba na kujenga  bweni zuri, gharama ya shilingi 86,482,000 ni gharama ndogo,nikilinganisha na maeneo mengine ambapo tumekuta miradi ya ujenzi wa mabweni. Mabweni yamejengwa kwa gharama kubwa,lakini hayajafikia kiwango na uzuri huu,kuna wilaya  ndani ya mkoa huu wa Manyara ambayo makadirio ya ujenzi wa bweni ni milioni 174,mpaka sasa wametumia milioni 89, lakini bweni halijafikia kiwango hiki.Natoa wito kwa halmashauri nyingine waje wajifunze Kiteto’’.


 Wilayani Kiteto  Mwenge  wa Uhuru  umepokelewa katika kijiji cha Ndaleta, baada ya mapokezi ,umekimbizwa umbali wa kilometa 108,  ambapo umepita katika tarafa 4 ,kata 10 , vijiji 20, na na kukesha katika uwanja wa michezo wa Kibaya .Wakati wa mbio hizo jumla ya miradi 5 imepitiwa, kati ya hiyo , miradi 2 imefunguliwa ,miradi miwili imewekewa jiwe la msingi, na mradi mmoja wa utunzaji mazingira,ambapo katika mradi wa utunzaji mazingira, zoezi la upandaji miti limefanyika katika shule ya sekondari Engusero.


Aidha thamani ya miradi yote ni shilingi za Kitanzania 6,996,805,804, ambapo wahisani wamechangia Sh. 6,411,919,000 /= ,jamii sh. 400,000,000,halmashauri ya wilaya Sh. 30,192,000/= na serikali kuu Sh.154,694,804/=.


Ujumbe wa mwenge wa uhuru mwaka 2018 ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha,wekeza sasa kwa maendeleo ya nchi yetu’.



.............MWISHO............

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa