• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mbunge Ataka Takwimu Sahihi za Mifugo Kiteto

Imetumwa : April 2nd, 2018

Mbunge wa jimbo la Kiteto Mhe.Emmanuel Papian akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akitoa maelekezo ya serikali  katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel  akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri .

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Tamim Kambona akijibu hoja za Wahe. Madiwani katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri . Aliyekaa  upande wake wa Kulia ni Mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Lairumbe Mollel na upande wake wa kushoto ni  katibu wa CCM (W) ya Kiteto Ndg. Shekue Pashua.

Wahe. Madiwani  wakiendelea na kikao cha baraza ndani ya  ukumbi wa  halmashauri ya wilaya ya Kiteto .


…………….HABARI KAMILI……………




Mbuge wa jimbo la Kiteto Mheshimiwa Emanuel Papian   ametaka kuwepo kwa Takwimu sahihi za mifugo wilayani Kiteto ili kuokoa  maisha ya wafugaji .Mheshimiwa Papian ameyasema hayo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mwishoni mwa  wiki.


Mheshimiwa Papiani amesema  kwamba halmashauri inatakiwa kufanya jitihada za haraka katika kupata takwimu halisi za mifugo. Akisisitiza kuhusu umuhimu wa wilaya kuwa na takwimu sahihi za mifugo  Mhe. Papian amesema “ Tutakapokuwa hatujapata takwimu halisi za mifugo,mtu ana ng’ombe 1000 ameandikiwa ng’ombe 500,serikali itakapokuja kukagua ikakuta ana mifugo 1000, ndipo udalali utakapo anza auction mart atasimama, ng’ombe  zitapigwa mnada, wafugaji wetu watapata hasara”.


Vilevile Mhe Papiani amesema kwamba takwimu za mifugo  ni muhimu sana katika kuwasaidia wafugaji kupata huduma stahiki za mifugo yao kutoka serikali kuu. Akisisitiza kuhusu umuhimu huo,Mhe Papian amesema “Kwa kupata takwimu sahihi za mifugo inatusaidia kupata namna ya kusukuma kupata hela kutoka serikali kuu za kuja kuchimba mabwawa na kufanya shughuli  nyinginezo za mifugo.Kwa hiyo tunapotoa takwimu ndogo, hata serikali kuu inafanyia kazi hizo hizo takwimu ndogo.Kumbe maeneo yenye mifugo mingi ndiyo yalitakiwa yapewe kipaumbele katika kuchimbiwa mabwawa ,majosho na ukarabati wa vitu vingine”.


Aidha  Mhe .Papian ametoa ushauri kwa Wahe. madiwani kwamba washirikiane na watendaji wa vijiji,wenyeviti wa vijiji na makatibu tarafa kuwaita wafugaji na kufanya nao  hesabu ya idadi ya mifugo walio nayo na idadi ya mifugo iliyopigwa chapa,ili wapate idadi halisi, na idadi hiyo ipelekwe katika ofisi ya mkurugenzi  wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa usalama wa wafugaji wanaoishi Kiteto.


Naye  mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mhe. Lairumbe Mollel ameunga mkono ushauri wa Mhe. Papiani , ambapo  amesema “Anachozungumza Mhe. mbunge ni kweli ,ni kwamba, hivi kama mtu  akisema anataka kuchimba mabwawa Kiteto , atachimbaje kama hatuna takwimu halisi za mfugo? Ili tupate dawa za ruzuku,tupate  mabwawa , na hata maeneo ya kulishia mifugo ni lazima tutoe takwimu halisi za mifugo iliyopo wilayani kwetu”.


Kikao hicho cha baraza la madiwani  katika siku yake ya pili kimejadili ajenda tisa, ajenda ya tatu ikiwa ni kupokea maelekezo ya serikali ambapo mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa ametoa maelekezo juu ya masuala mbalimbali likiwemo suala la elimu,uandikishaji wa vitambulisho vya taifa , utaratibu wa uchomaji  na uuzaji mkaa pamoja na upandaji miti.




…………… MWISHO……………

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa