Mbunge wa Kiteto Mhe. Emmanuel Papian akizungumza na wakazi wa pori namba moja katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo hilo mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Kitongoji akifungua Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kimana, eneo la Pori namba moja mwishoni mwa wiki.
Katibu wa CCM(W) Ndg Shekue Pashua akiwasalimia wakazi wa pori namba moja katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kimana, eneo la Pori namba moja mwishoni mwa wiki.
Afisa mipango (W) ya Kiteto bibi Beatrice Lumbeli akiwasalimia wakazi wa pori namba moja katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kimana, eneo la Pori namba moja mwishoni mwa wiki.
Wakazi wa Pori namba moja wakiwa wamekusanyika kumsikiliza Mbunge wao Mhe. Emanuel Papian katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la pori namba moja mwishoni mwa wiki.
Wakazi wa Pori namba moja wakiwa wakiwasilisha kero kwa Mbunge wao Mhe. Emanuel Papian katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la pori moja mwishoni mwa wiki.
..............HABARI KAMILI.............
Mbunge wa Kiteto Mheshimiwa Emanuel Papian amewataka wakazi wa Kijiji cha Kimana, Kitongoji cha Nabirikunya eno maarufu kama pori namba moja kujenga nyumba bora. Mhe Papian ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika katika eneo hilo mwishoni mwa wiki.
Akizungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Papian amesema kwamba wakazi wa eneo hilo wanatakiwa kujenga nyumba bora, na si hivyo tu, bali wanapokuwa wakijenga wazingatie mpangilio unaotakiwa ili kuruhusu huduma nyingine kama vile zima moto na umeme kuweza kufika katika mitaa yote ya eneo hilo kwa urahisi.Akisitiza kuhusu ujenzi wa makazi bora Mhe. Papian amesema“ Tunataka hapa papangike, nyumba bora zijengwe, ili umeme uweze kuletwa hapa, mfanye shughuli za maendeleo,Nyumba za nyasi hapana.Mmeletwa hapa mkae usawa wa barabara. Eneo hili ni la kudumu, jengeni makazi bora ,fanyeni shughuli za maendeleo na muishi kwa amani. Mkishajipanga vizuri ,mkajenga makazi bora, yaliyopangwa vizuri tutawaletea huduma zote muhimu hapa”
Katika hatua nyingine Mhe. Papian ameweka mkazo katika suala la elimu, ambapo amewataka wakazi wa eneo hilo kutokubali kukaa na watoto majumbani ,bila kuwapeleka shule,kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu. Akisisitiza kuhusu hilo Mhe. Papian anasema”Sasa hivi kuna mavuno, mwenyekiti wa kitongoji, changeni, mjenge madarasa, mkifikisha madarasa matatu ,nendeni kwa Mkurugenzi ombeni shule isajiliwe, ikishasajiliwa mimi pamoja na serikali tutaongeza nguvu kujenga madarasa mengine, eneo hili kitakuwa na shule”.
Katika mkutano huo wananchi wamewasilisha kero mbalimbali,ambapo Mhe. Papian ametoa majibu kuhusiana na kero hizo na kuahidi kuzifanyia kazi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi, sambamba na hayo Mhe. Papian ametoa rai kwa wananchi hao kuishi kwa kuheshimiana na kwa upendo ili amani iendelee kutawala katika eneo hilo.
Mhe. Papian yuko katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika vijiji mbalimbali jimboni mwake. Ziara hiyo inafanyika kwa muda wa siku saba,ambapo katika siku ya kwanza ya ziara yake hiyo, miongoni mwa vijiji alivyovitembelea ni kijiji cha Kimana,kitongoji cha Nabirikunya, eneo la pori namba moja.
..........MWISHO............
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa