Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mheshimiwa Edward Olelekaita amekabidhi jumla mifuko 600 ya saruji kwa taasisi mbalimbali zilizopo jimboni kwake.
Makabadhiano hayo ambayo yamefanyika katika Hospitali ya Wilaya Kiteto, Septemba 12, 2023, yalihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo wataalamu kutoka Halmashauri, madiwani, watendaji wa kata pamoja na wenyeviti wa mitaa.
Akizungumza kuhusu makabidhiano hayo Afisa Mipango wa Wilaya Bwana Erasmo Tellun Ndelwa alisema kwamba saruji zilizokabidhiwa ni sehemu tu saruji ambazo Mh. Olelekaita alikua akiahidi akiwa katika ziara zake mbalimbali katika mwaka 2022/2023.
Taasisi zilizonufaika na mgao huo katika awamu ya kwanza ni shule za msingi 10 ambazo zimepokea jumla ya mifuko 520, zahanati ya Ndirigishi ambayo imepokea mifuko 50, shule ya sekondari Eco ambayo imepokea mifuko 20 na Kituo cha Polisi Wilaya, Kibaya ambacho kimepokea mifuko 10.
Nae mmoja wa Watendaji wa Kata, Bwana Stephen Alphonce Stephen ambaye ni Mtendaji ya Kata ya Kaloleni alimshukuru Mh Mbunge na kusema kwamba amewapunguzia gharama katika kufanya ukarabati wa shule. Amesema kwamba mifuko 35 ya awali waliyoipokea kwaajili ya shule ya msingi Kaloleni, itawasaida katika kufanya marekebisho katika vyumba vya madarasa ya shule hiyo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa