Mbunge wa jimbo la Kiteto Mhe. Emmanuel Papian akizungumza kabla ya uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo.
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa , Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri, Kamati ya ulinzi na Usalama,Wakuu wa idara za Halmashauri ,watumishi wa Halmashauri pamoja na idara na taasisi mbalimbali wakiwa tayari kwa uzinduzi wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo.
Mbunge wa jimbo la Kiteto Mhe.Emmanuel Papian akiwa amemshika mkono mfanyabiashara mdogo kama ishara ya kumpongeza ,baada ya mfanyabiashara huyo kupewa kitambulisho.
Wafanyabiashara wakiwa wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya kupata vitambulisho.
.................HABARI KAMILI...............
Mbunge wa Kiteto Mheshimiwa Emmanuel Papian amewataka wafanyabiasha kulipa kodi ili serikali iweze kuleta maendeleo.Mhe Papian ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji vitambulisho vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli kwa wafanyabiashara wadogo.Uzinduzi ambao umefanyika Kibaya mjini, katika eneo lijulikanalo kama chini ya mti mwishoni mwa wiki.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Papian amewataka wafanyabiashara hao kuwaza kukua ili wafike mahali walipe kodi kama wafanyabiashara wengine.Akisisitiza kuhusu kulipa kodi Mhe. Papian amesema “Sisi tunafurahi kwamba leo watu wanakwenda kupata vitambulisho kwa sababu ni wajasiliamali wadogo,lakini ni matumaini yetu kwamba baada ya muda mtakuwa muelekee pale TRA mlipe kodi.Rais ametoa vitambulisho, na sisi tunasimamia mtapewa ,tunahitaji wafanyabiashara wa Kiteto wakue na wasonge mbele,walipe kodi tupate maendeleo”.
Mhe Papian pia amesema kwamba maendeleo ambayo serikali imekuwa ikiyafanya yanatokana na kodi,hivyo hakuna namna ambayo mtu anaweza akaishi bila kulipa kodi,kwa sababu kulipa kodi ni lazima, ili nchi iweze kujiendesha na kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha Mhe. Papian amewataka wafanyabiashara ambao tayari ni walipa kodi TRA kutochukua vitambulisho hivyo kwa sababu watavitumia kukwepa kulipa kodi,badala yake , wale waendelea kulipa kodi, kwani vitambulisho hivyo sio kiwango chao,bali ni vya wafanyabiashara wadogo,ambao hawajafikia kiwango cha kulipa kodi TRA.
Sambamba na kuwataka wafanyabiashara kulipa kodi, Mhe. Papian ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilaya ya Kiteto kuacha kufunga biashara za watu,kwani kwa kufanya hivyo kodi haiwezi kupatikana, bali wawaite wafanyabiashara, wakae nao meza moja wazungumze.Amesema kwamba mazungumzo ni njia bora zaidi itakayosababisha ukusanyaji wa mapato bila kuathiri upande wowote .
Katika hatua nyingine Mhe Papian amesema kwamba ni vema TRA ishirikiane nae yeye pamoja na viongozi wengine, na wadau wa maendeleo waliopo wilayani hapa ili wawasaidie kubaini vyanzo vingine vya mapato, kwani viko vyanzo ambavyo wao wanavifahamu ,hivyo kwa kushirikiana nao,vyanzo vipya vinaweza kuwekwa bayana na kusababisha ongezeko katika ukusanyaji mapato.
Zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo litaendelea katika ofisi ya biashara ya halmashauri, ili wafanyabiashara wote wanaostahili kupata vitambulisho hivyo wapate.
.............MWISHO.............
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa