• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara A.Mnyeti Aipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa Kupata Hati Safi.

Imetumwa : May 30th, 2020

Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander .Mnyeti Akizungumza Katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Kilichofanyika Katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mjini Kibaya Tarehe 28.05.2020.

Kutoka Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi.Beatrice Rumbeli, wapili ni Mh.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel na watatu ni Mh.Mwenyekiti wa CCM Wilaya Omari Kiondo.

Mh.Mbunge wa Wilaya ya Kiteto Emmanuel Papian Akisalimia Wajumbe wa Baraza Hilo.

Hao hapo juu ni Waheshimiwa Madiwani Wakiwa katika Kikao Hicho



Mh.Diwani Viti Maalumu Chadema Zamzam Said Akizungumza Wakati Anatoka Chadema Kuhamia CCM Siku Hiyo Hiyo ya Kikao cha Baraza la Madiwani Mbele ya MH. Mkuu wa Mkoa wa Manyara A. Mnyeti.

Mh.Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kiteto Omari Kiondo (aliyevaa shati la kijani)  akikabidhiwa Kadi ya Chadema na Mh.Diwani Viti Maalumu Chadema Zamzam Said (kulia mwenye kitambaa cheupe) Ambaye amehamia Rasmi Kuingia CCM, wa Katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Kiteto Bi.Neema Nyalege


Waheshimia Madiwani na Wajumbe Mbalimbali Walisimama Kama Ishara ya Kumpongeza na Kumpokea Mh. Diwani (Viti Maalum) Zamzam


--------------------------------------  HABARI KAMILI -----------------------------------------



Mh.Mkuu wa Mkoa wa  Manyara, Alexander Mnyeti ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo katika uongozi wake  kwa miaka ya fedha ya  2016/17,2017/18 na 2018/19 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali.

Mh.Mkuu wa Mkoa wa  Manyara, Mnyeti alitoa pongezi hizo akiwa katika ziara ya kuhudhuria Baraza la Madiwani kwa kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali yaliyofanyika katika makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mjini Kibaya tarehe 28.05.2020.

“Kwa kweli lazima niwapongeze Waheshimiwa Madiwani, Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel, Mh.Mkuu wa Wilaya  Mhandisi T. Magessa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona, Wakuu wa Idara na Vitengo na Wataalam wote wa Halmashauri kwa kuhakikisha mnapata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo kwani miaka ya nyuma hali haikuwa kama ilivyo sasa, hongereni sana” Alisema Mh.Mkuu wa Mkoa huyo.

Pamoja na pongezi hizo pia alimtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali kuhakikisha baadhi ya hoja kama za upungufu wa watumishi na kupewa ukuu wa Idara/Kitengo zinaondolewa kwa Halmashauri kwa kuwa hizo ni hoja za kisera na kamwe hazihusiani na Madiwani kwani Madiwani hawana uwezo wa kutatua tatizo la upungufu katika Halmashauri.

Aidha Mh. Mkuu aliendelea kwa kusisitiza, “Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali kuna baadhi ya hoja kwa kweli ni vema mkawakague Wizara ya Utumishi na TAMISEMI ndo muwaulize kwanini hawaleti watumishi na kuwapandisha vyeo watumishi waliokaimu Idara/Vitengo kwa muda mrefu Mkoa wa Manyara” Akijibu hoja hiyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali  Mkoa wa Manyara Bwana Paschal Mawago alisema kuwa watajitahidi kukaa na wataalam wa Halmashauri kuhakikisha kuwa hoja zote za kisera zinafutwa na pia aliwataka wataalam kufika katika Ofisi za Mkaguzi zilizopo Babati wakati wowote wapatapo vielelezo vya baadhi ya hoja ili kuzifuta na kuzifunga.

Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuwa juu zaidi kwa kuvuna wanachama mbalimbali toka vyama vya upinzani kwani katika Baraza hili la Madiwani Wilayani Kiteto Mh.Mkuu wa Mkoa alishuhudia Diwani wa viti Maalum Mh. Zamzam Said  kutoka CHADEMA alitumia nafasi hiyo kukihama chama chake na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Mheshimiwa Mwenyekiti kuanzia leo tarehe 28.05.2020 mimi nikiwa kama Diwani wa CHADEMA nimeamua kujiunga na CCM bila kushawishiwa na mtu yoyote kwani sioni jambo la maana watakalofanya CHADEMA ambalo Mheshimiwa Rais  John Pombe Magufuli hajafanya. Alisema Mheshimiwa Zamzam.

Mh.Mkuu wa Mkoa pia alitumia ziara hiyo kuwaaga na kuwatakia kila la heri  Madiwani na Wabunge wote wa Mkoa wa Manyara kwani Mabaraza yote ya Madiwani yanayotarajiwa kuvunjwa kuanzia tarehe 10 .06.2020 ili kupisha mchakato wa uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais kuanza. pia aliwataka Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia ipasavyo rasilimali za Halmashauri katika kipindi hicho ambacho Halmashauri hazitakuwa na Mabaraza ya Madiwani.

“Kwa kuwa hili ni Baraza la mwisho kabla ya Baraza kuvunjwa nitumie nafasi hii kuwatakia kila la heri Madiwani katika uchaguzi ujao wa mwezi Oktoba, naamini zaidi ya 90% mtarudi baada ya uchaguzi, lakini  katika kipindi hiki nawataka Mh. Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara na Vitengo kusimamia ipasavyorasilimali zote ili kuhakikisha mnadhibibiti matumizi ya fedha” Alisisitiza Mh. Mkuu wa Mkoa huyo.



Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa