Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera Akabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona Msaada wa Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Sh. Milioni 99,983,700/=Toka Shirika la Hifadhi ya Jamii PPF Katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.
Imetumwa : May 27th, 2017
Kutoka Kushoto ni Mh. Diwani Paulo Tunyoni Aliyehudhiria kwa Niaba ya Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri (W), Anayefuatani Katibu wa CCM (W) Bw. Pasua, Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa, Kisha Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr. Joel N. Bendera, Afisa Uhusiano wa PPF Kanda ya Kazkazini Bibi. Lulu, Anayefuata Wakiume ni Meneja wa PPF Kanda Kaskazini.
wa Mwisho Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona.
Katibu Tawala WIlaya ya Kiteto Bw. Ndaki S. M. Akiwatambulisha Wageni Mbalimbali Waliohudhuria Hafla Hiyo.
Mh. Diwani wa Kata ya Kibaya Akiwasalimia Wananchi.
Mh. Diwani C. Parmet Aliyehudhuria kwa Niaba ya Mh. Mbunge Jimbo la Kiteto Akiwasalimia Wananchi.
Katibu wa CCM (W) Kiteto Bw. Pasua Akiwasalimia Wananchi.Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona Akiwasalimia Wananchi.
Mh. Diwani Paulo Tunyoni Aliyehudhiria kwa Niaba ya Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri (W), Akiwasalimia Wananchi.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa Akiwasalimia Wananchi.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii PPF Bibi. Lulu Akifafanua Jambo.
Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera Akihutubia Wananchi na Watumishi Mbalimbali Wilayani Kiteto.
Wananchi Mbalimbali Waliohudhuria Katika Hafla Hiyo.
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr. Joel N. Bendera Akikabidhiwa Vifaa Tiba Hivyo Toka kwa Afisa Uhusiano wa PPF Bibi. Lulu.
Kutoka Kushoto Mh. Diwani C. Parmet Aliyehudhuria kwa Niaba ya Mh. Mbunge Jimbo la Kiteto,
Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera (wa katikati) na Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto
Bw. Tamim H. Kambona (wakulia) Wakielekea Kwenye Mradi wa Jengo la MAMA NGOJEA Ambalo Kina Mama Wajawazito Watakuwa Wakisubiri Humu Kabla ya Kuingia Katika Chumba cha Kujifungulia kwa wale Wanaotoka Mbali na Hospitali Hii ya Wilaya Kiteto.
Bibi. Elizabeth Kiula Akitoa Maelezo Kuhusu Mradi Huu na Matumizi yake
kwa Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona Akifafanua Kuhusu Mradi Huu kwa
Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Mkoa Dkt Joel N. Bendera.
HABARI KAMILI ....
Katika muendelezo wa PPF kuchangia huduma mbalimbali imetoa Vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 99,983,700 ambavyo vyote hivi vimenunuliwa kutoka Shirika la umma la Madawa (MSD) navyo ni Vitanda viwili (2) vya kujifungulia,Vitanda vya kawaida vitano (5) na mashuka hamsini na tatu (53) ya wagonjwa na mipira maalumu ya akina mama hamsini na sita (56). Wao kama PPF wanaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya tano ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania J. P. Magufuli katika kumhudumia mwananchi kwa kuboresha huduma za afya nchini kwa kuondoa kero kwa wananchi wetu.
PPF WOTE SCHEME ni mfumo maalumu wa kuchangia unaozihusiaha sekta isiyo rasmi pamoja na ule mfumo wa ziada uliopo kwenye sekta iliyo rasmi. Hivyo PPF wanatoa huduma kwa kila mwananchi bila kubagua kuanzia Mfanyakazi, Mkulima, Mfugaji kwa hiyo siyo tu aliyeajiliwa hata ambaye amejiajili mwenyewe anaweza kujiunga na PPF kwa maisha yako ya sasa naya baadaye mafao ya ulemavu, wategemezi, kiinua mgongo, elimu, uzazi ndiyo maana pia kipaumbele ni kwa akina mama na wajawazito. Mh. Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Magessa Katika kanda hii ya Kaskazini yenye Mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga sisi ndiyo wa kwanza, kwa kuwa na wanachama zaidi ya 1000 hivyo kuchangia kwetu ndiyo kumekuja na manufaa haya mnayoyaona. Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera alisema kuwa PPF iko hapa kwa ajili ya kutukomboa hivyo kila mmoja wetu ajipange kuingia kwani mgao wanaoutoa kwa wananchi ni jambo zuri la kimaendeleo linalopaswa kuigwa na Mifuko mingine. Fedha zilipaswa kutengwa kununua vifaa hivi kwa Halmashauri (W) sasa itaelekezwa katika maeneo mengine ya manufaa kwa Afya kama vile uboreshaji wa miundombinu ya upatikanaji wa Maji.
Anaamini kabisa kila mtu kama atajituma katika kazi sisi tukakuwa ni nchi ya kutoa na siyo kuomba misaada. Watu wasiwe wabadhilifu na kufanya kazi bila kujali wakati ni shida kwani nchi yetu siyo maskini ni tajiri. Kwa hiyo tuungane mkono na ambaye amezoea kufanya kazi kwa mazoea yaani kwa kimombo “business as usual” haendi na wakati hivyo aachie ngazi.
Mgeni Rasmi Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera amewashukuru PPF kwa kuisaidia Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto katika kusukuma maendeleo kupitia afya kisha alikabidhi kadi moja kwa niaba ya waliojiunga na PPF WOTE SCHEME ambaye ni Mh. Diwani Bibi. Laizer Ngaisi Michael.
Mwakilishi wa PPF Bibi Lulu, amemshukuru sana Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt. Joel N. Bendera kwa kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Kiteto wanaunga mkono kwa kujiunga na kuchangia PPF kwa kishindo.Mwakilishi huyo alisema wanapotoa mchango kwa jamii wanafata sera ya uwekezaji ya PPF na huu ni mwanzo ila wataendelea kushirikiana na kuwa karibu na wananchi ili kuhakikisha kuwa wanachangia huduma ya PPF na kupata huduma bora za Afya.
Hakukuwa na Mzaha Kwani Wananchi Wamevutiwa na Wanajiunga kwa Wingi Baada ya Kuona Manufaa ya PPF WOTE SCHEME. Wawakilishi wa PPF Wakiwa Katika Zoezi la Usajili wa Wanachama Hapo Hapo Kwenye Hafla Hiyo.
Maelekezo ya kujiunga na PPF WOTE SCHEME.
Kujiunga ni bure kwa kupigwa picha kisha utapewa kitambulisho chenye namba ya utambuisho wako hapo ndipo utaanza rasmi kuchangia. Uchangia huu ni kuanzia shilingi elfu 20,000/= tu kila mwezi. Pia taarifa zote na uchangiaji huu unaweza kufanyika katika simu yoyote na mahali popote kwa kutumia Mpesa, Tigo Pesa na Airtel money.
Kuanzia kesho Jumapili ya tarehe 28.05.2017 wamejipanga kutembelea Kata kadhaa ikiwamo Sunya, Kibaya, Njoro, Kijungu, Matui, Engusero na Ngipa. Hata hivyo waliojiunga kipindi cha nyuma na hawakupata vitambulisho vyao vipo Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto, Idara ya Maendeleo ya Jamii (W).
Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona Akizungumza Jambo Baada ya Kupokea Vifaa Husika.
Mwisho,
Mkurugenzi Mtendaji (W) Bw. Tamim H. Kambona alimshukuru Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr. Joel N. Bendera na kutamka kuwa tumevipokea vifaa hivi vikiwa safi na salama lakini nikuhakikishie sisi Halmashauri (W) tunakuhakikishia tutavitunza vifaa hivi ili kila siku viendelee kuwa katika hali nzuri, hivyo jukumu la usafi na kuvitunza ni la kwetu sasa. Aliwashukuru PPF kwa msaada walioutoa na waendelee kutoa misaada kama hii katika Wilaya hii.