Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Songea Mwenye Suti Akizungumza na Viongozi Hao Katika Ukumbi wa Maktaba ya Wilaya ya Kiteto, Kulia Kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Emmanuel Mwagala na Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Bi. Neema Nyalege.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona Aliyesimama Akizungumza Katika Kikao hicho, Kushoto Kwake ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Songea na Mwisho ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Bi. Neema Nyalege.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Bi. Neema Nyalege Aliyesimama Akizungumza Katika Kikao hicho
Viongozi mbalimbali Wakiwa Katika Kikao Hicho Kama Wanavyoonekana Kwenye Picha za Hapo Juu.
---------------------------------------- HABARI KAMILI ----------------------------------------
Haya yamejiri katika kikao cha viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto yakiwahusisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji yaliyofanyika katika ukumbi wa Maktaba ya Wilaya Kiteto. Mkuu wa Wilaya huyo amesema "Kila mmoja anapaswa awe ana taarifa zote za ofisi yake ikiwa ni pamoja na kuwajua watumishi alionao kwa utendaji wao wa kazi kwa ujumla".
Baada ya majadiliano na viongozi hawa kuhusiana na baadhi ya migogoro ya ardhi, ilifahamika kwamba Sheria ya aridhi iko wazi juu ya mipango ya matumizi bora ya ardhi na iko vizuri chamsingi kwa viongozi ni kufuata taratibu za maamuzi ya maeneo yoyote katika kijiji kuamuliwa na mkutano mkuu wa kijiji kama sheria ya adhi ya namba 5 ya mwaka 1999 inavyoeleza, kisha mihutasari ya mikutano hiyo ndiyo msingi na dira ya mustakabali wa nini cha kufanya katika kijiji husika. Hata hivyo inajulikana kuwa daftari la wakazi au rejista ya wakazi ni muhimu kuwepo, kutekelezwa na kusimamiwa kisheria hili litasaidia kujua kila mtu katoka wapi, anakaa wapi na anafanya nini kwa madhumuni gani.
Kwa sasa kasi ya utendaji wetu wa kazi haujaridhisha hivyo inatupasa kuongeza kasi zaidi, ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogowadodgo ni muhimu wapewe wote wanaostahili kama agizo la Mh. Rais Dkt. J. P. Magufuli alivyoagiza kwani hadi sasa wapo wajasiriamali ambao hawana hadi leo vitambulisho hivi, kwa hiyo mjitahidi wale wote wenye sifa za kupata vitambulisho wapewe haraka.
Maafisa Watendaji katika ngazi zote mkae katika maeneo yenu ya kazi siku zote, zingatieni kufungua ofisi za serikali na kufunga kwa muda mwafaka, tuwahudumie wananchi hawa kwani ndiyo wajibu wetu kwao na kwa serikali pia, cha msingi ukiwa kama kiongozi weka ratiba ya siku zipi katika wiki utakuwepo ofisini na zipi utakuwa kwenye miradi na kutembelea kazi mbalimbali za maendeleo ya vijijini.
Mh.Mkuu wa Wilaya huyo aliendelea kusisitiza kwamba "fanya kazi lakini hukatazwi kufanya kazi baada ya masaa ya kazi hili ni la kawaida ili kujiongezea kipato kama vile ufugaji na kilimo lakini kumbuka kujiongezea kipato ambacho ni halali, usitoroke kazini kwenda kufanya kazi zako mwenyewe. Suala la Kutilia mkazo ni kuwashawishi wananchi kujiunga katika bima ya afya ya jamii, ni muhimu sana kwani mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe lakini ni lazima mtu huyu awe na afya bora ndipo atazalisha kwa ufanisi.
Zamani watu wote waliokuwa wakimaliza masomo ya kidato cha 4 walikuwa wanaajiriwa wote bila shida lakini leo hii kuna changamoto nyingi za kupata ajira na vyuo ni vingi sana na wahitimu ni wengi mno ni maendeleo kwa kweli, kwa sasa tunapaswa kama wazazi, kama viongozi kuwaandaa watoto wetu hawa kuwa wajasiria mali na sio kutegemea kazi za maofisini "white collar job" kwani ukimuandaa mtoto kujiajiri baadaye hatapenda tena kazi za kuajiriwa atajitafutia yeye mwenyewe kazi na wazazi hatutahangaika tena na uzuri nchi yetu ni pana na yenye amani, mzunguko wa fedha upo vizuri, miundombinu wezeshi ipo barabara, usafirishaji, mawasiliano na vingine vingi hivyo fursa hizi zitumike kwa wao kujiajiri ipasavyo.
Tukumbuke kudumisha utawala bora kwa kuzingatia kusoma mapato na matumizi katika ngazi zote za mikutano mikuu ya kitongoji na kijiji pia ili kuongeza imani ya wananchi kwa serikali yao hii itarahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yao kupitia muitikio chanya wa utoaji wa michango na usimamizi wa miraji mbalimbali ya kijiji husika kupitia kamati zao.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa