Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa (aliyevaa suti) Wakati wa Makabidhiano Hayo na Maafisa Tarafa Hao Tarehe 13.05.2020
Kulia kwake ni Afisa Tarafa wa Makame Bw. Ibrahimu Olemario na kushoto kwake ni Afisa Tarafa wa Olboloti Bw.Fadhiri Alexander
Wa kwanza kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Bi. Neema Nyalege
-------------------------------------------------------- TAAFIFA KAMILI ---------------------------------------------------
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto huyo, Mhandisi Tumaini Magessa alikabidhi Pikipiki hizo kwa hawa wafuatao , kwa majina ni; Bi.Dhulpha Laizer Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kibaya, Bw.Fadhiri Alexander Afisa Tarafa wa Tarafa ya Olboloti, Bw.Jeremia Mwangaza Afisa Tarafa wa Tarafa ya Dosidosi, Bw.Amedeus Kitira Afisa Tarafa wa Tarafa ya Sunya, Bw.Ibrahimu Olemario Afisa Tarafa wa Tarafa ya Makame, Bw. Nivile Komolo Afisa Tarafa wa Tarafa ya Matui na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Kijungu Bw.Julius Laizer.
Mh.Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa amewataka Maafisa Tarafa hao kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kutumia vyombo hivi vya usafiri kuongeza kasi ya kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao Wilayani Kiteto.
Aidha, Mh.Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhandisi Tumaini Magessa amemshukuru sana Mh.Rais Dkt J.P. Magufuli kwa kutimiza ahadi yake aliyoitoa mwaka jana 2019 kwa Maafisa Tarafa hawa ya kuwapa vyombo vya usafiri ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao mbalimbali.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa