Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema Emmanuel, ameweka Mawe ya Msingi katika miradi mitatu wilayani hapa.
Miradi hiyo ni pamoja na Jengo Jipya la Zahanati ya Ngabolo, Shule ya Msingi ya Mkondo mmoja ya Oloimugi pamoja na Daraja Barabara ya Kibaya-Mbeli.
Miradi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru siku ya tarehe 13 Julai 2025.
Aidha katika siku hiyo, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuweka Jiwe la Msingi katika mradi wa Ujenzi wa Ghala la kihifadhi mazao.
Sambamba na hayo, Mwenge wa Uhuru 2025 unatarajiwa kutembelea Mradi wa Kikundi cha Vijana Weredi Studio, Mradi wa Uboreshaji Miundombinu na Usmbazaji wa Maji Kibaya Mjini na pia kutembelea Shughuli za Mapambano Dhidi ya Changamoto za Lishe.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa