Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, Januari 27, 2025 ameungana na wakazi wa Wilaya ya Kiteto katika shughuli ya upandaji wa miti ikiwa ni ishara ya kuadhimisha kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maadhimisho hayo ambayo yamehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Manyara wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji na Makatibu Tawala wa Wilaya, yamefanyika katika viwanja vya jengo jipya la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kupanda miti 500 kuzunguka eneo hilo huku wananchi wakipata zawadi ya miti ya kivuli na matunda kwa ajili ya kupanda kwenye makazi yao.
RC Sendiga amewashukuru wananchi wa Kiteto kwa kuungana pamoja katika shughuli hiyo muhimu ya utunzaji wa mazingira.
"Hii imekuwa mara ya pili kwa Mkoa wa Manyara kuadhimisha kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mhe. Rais Samia Suluhu huku zoezi la upandaji miti likiendelea", amesema RC Sendiga.
Aidha, RC Sendiga wakati akitoa salamu za mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemshukuru Mhe Rais kwa kendelea kuelekeza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye manufaa chanya kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara.
Kauli mbiu ya Mkoa katika madhimisho hayo ni *"Upandaji Miti kwa Maendeleo Endelevu"* ilhali kauli mbiu ya Wilaya ni *"Kiteto ya kijani ipo Mikononi Mwetu"*
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa