Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MKURUGENZI ASISITIZA UBORA MIRADI YA UJENZI INAYOTEKELEZWA.

Imetumwa : May 4th, 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya KIteto, CPA. Hawa Abdul Hassan, amewagiza wasimamizi wa miradi ya ujenzi wilayani Kiteto kuhakikisha kuwa inatekelezwa kwa ubora unaotakiwa ili thamani ya pesa ionekane.

Hayo ameyazungumza katika ziara yake ya kukagua miradi Mei 4, 2024 akiwa ameongozana na Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi, Mkuu wa Idara ya  Elimu Sekondari, Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Mkuu wa Idara ya Mipango na Uratibu pamoja na wahandisi wa Ujenzi wa Halmashauri.

Katika kila mradi ambapo alipita kukagua, Mkurugenzi amesisitiza mambo matatu ambayo ni kuongezwa kwa kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati, ubora wa miradi hiyo pamoja na matumizi bora ya fedha (Value for Money).

Aidha amesema maelekezo hayo siyo kwa ajili ya miradi hiyo tu bali ni kwa miradi yote inayoendelea kutekelezwa wilayani Kiteto.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ndugu Godfrey Mwangairo, amesisitiza kufuata utaratibu wa serikali wa manunuzi ya umma katika mfumo wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NEST).

Ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo ilianzia katika Hospitali ya Wilaya kwa kukagua ukamilishaji wa mradi wa majengo matatu kisha kuelekea katika shule ya Msingi Chemchem na kukagua mradi wa vyoo matundu 11 na kutoa maelekezo ya kuanza kwa ujenzi wa chumba kimoja cha darasa katika shule hiyo. Maagizo hayo pia yametolewa katika shule ya Msingi Msente.

Aidha Mkurugenzi pamoja na timu yake alikagua ujenzi wa nyumba nne za wakuu wa idara pamoja na nyumba ya mkurugenzi zinazojengwa katika eneo la Bwagamoyo. Mkurugenzi huyo aliendelea na ziara yake katika Shule ya Sekondari Kiteto na kukagua ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa pamoja na ujenzi wa vyoo matundu manane shuleni hapo. Ujenzi wa chumba kimoja cha darasa pamoja na ukamilishaji wa boma la chumba  cha darasa katika Shule ya Sekondari Bwakalo pia ulikaguliwa katika ziara hiyo.

Vilevile Mkurugenzi huyo alipita kukagua ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Partimbo na pia kukagua ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na vyoo matundu manane katika Shule ya Sekondari Partimbo. Mradi kama huu pia unatekelezwa katika shule ya Sekondari Njoro ambapo timu hiyo pia ilifika kukagua.

Jumla ya miradi tisa ilikaguliwa katika ziara hiyo ya siku moja. Miradi yote hiyo ina jumla ya thamani ya TZS 1.9 bilioni ambapo ni fedha kutoka serikali kuu na pia kutoka Mapato ya Ndani ya Halmashauri katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • JAMII YAASWA KUZINGATIA HAKI ZA WATOTO.

    June 16, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa