Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona akabidhi Baiskeli Arobaini na Mbili (42) kwa Vikundi vya Mradi wa Kilimo cha Mbogamboga Wilayani Kiteto
Imetumwa : May 17th, 2017
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona ( aliyesimama ) Akizungumza na Wadau wa Mradi wa Kilimo cha Mbogamboga Wilayani Kiteto. Mwenye Koti Jeusi ni Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika (W) Kiteto Bw. Robert Urasa.
Mwakilishi wa Shirika la Watafiti wa Mbogamboga ( AVRDC ) Bibi. Sofia Bongole Akiwasilisha Mada iliyohusu Teknolojia ya Mbogamboga kwa WadauMbalimbali Waliohudhuria.
Mwenye Koti Jeusi Kulia ni Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya - Kiteto Bw. Robert Urasa Akitoa Maelezo Juu ya Mradi Huu kwa Wadau.
Baiskeli kabla ya kugaiwa Kwa Vikundi Hivyo ni Hizo Hapo Juu.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji (W) Kiteto Bw. Tamim H. Kambona ( aliyevaa suti ya kijivu ) Katika Zoezi la Kukabidhi Baiskeli Hizo Makao Makuu ya Wilaya ya Kiteto,
kulia mwenye koti jeusi ni Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya - Kiteto Bw. Robert Urasa.
Baadhi ya Wadau Hao wa Vikundi vya Mbogamboga Waliokuwa Wamefurai Baada ya Kupewa Bure
Vyombo Hivyo vya Usafiri Wakiendesha Baiskeli Hizo Katika Makabidhianao Hayo..
HABARI KAMILI .....
MRADI WA KILIMO CHA MBOGA MBOGA MANYUMBANI “HOME GARDENING PROJECT”
Mradi unaojishugulisha na Usambazaji wa Teknolojia Bora za Kilimo cha Mbogamboga unaotekelezwa Wilayani Kiteto na Taasisi ya Watafiti wa Mbogamboga (AVRDC), iliyopo Jiji la Arusha kupitia Mradi wa “Feed the Future” unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Serikali ya Marekani (USAID), Ofisi ya Tanzania kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Lengo la Mradi - Kupunguza udumavu na athari katika afya kwa kundi la watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5) na wanawake wenye umri kati aya miaka 14 - 35
- Kuongeza kipato cha Kaya
- kutoa elimu kwa walengwa na kuwawezesha katika kuboresha uzalishaji na matumizi ya mazao yenye virutubisho vingi jamii ya mbogamboga za asili.
Uanzishwaji wake.
Mradi huu ulianzishwa Wilayani Kiteto mwaka 2015 hadi sasa unaendelea kuhudumia na kunufaisha wananchi.
- Kwa awali 2015 vilikuwa Vijiji vitatu tu (3) ambavyo ni Ngipa, Kijungu na Kibaya.
- Kwa mwaka wa pili 2016 tuliongeza Vijiji tisa (9) ambavyo ni Loolera, Zambia, Mwitikira, Engusero, Orkine, Emarti, Njoro, Chang’ombe (Njoro) na Chapakazi.
- Kwa mwaka wa tatu 2017 Halmashauri kwa kushirikiana na Wadau wa Mradi huu tumezidi kuongeza idadi ya Vijiji vingine saba (7) yaani Ndaleta, Mwanya,
Songambele, Magungu, Dosidosi, Kimana (Kitongoji cha Mbeli) na Mji Mdogo wa Matui.
- Hivyo kupelekea jumla ya Vijiji 19 kunufaika na Mradi huu.
Huduma zinazotolewa kwa Vikundi ambazo ni mafanikio makubwa katika Mradi huu ni hizi zifuatazo:-
- Kutoa mafunzo kuhusu uzalishaji wa mbogamboga kupitia mashamba darasa ya eneo maalumu kwa kila Kijiji na Kata.
- Mafunzo juu ya mapishi ya mbogamboga pasipo kuathiri virutubisho vyake.
- Kuwapatia mbegu bora za baadhi ya mbogamboga za asili Mnavu, Bamia, Kunde, Mlenda Ngogwe, Mgagani na Mchicha.
- Kuwapatia usafiri aina ya Baiskeli ili kurahisisha kazi za usimamizi na uelimishaji katika ngazi ya Kaya kwa Vikundi husika kwa kila Kata na Kijiji ambapo leo Mei 2017 baiskeli
zilizotolewa ni arobaini na mbili (42).
Vikundi hivi vimewashuruku sana Wafadhili hawa na Halmashauri (W) Kiteto katika kuwawezesha hadi kufikia hatua waliyonayo sasa ambayo ni endelevu na imeonyesha matokeo chanya kiafya na kiuchumi katika jamii na familia zao.