Aliyeshika "mic" ni Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw.Tamim Kambona Akizindua Kampeni ya Usafi wa Mazingira Kata ya Njoro
Aliyeshika "mic" ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Njoro, Kata ya Njoto Wilaya ya Kiteto Mh. Saidi Athumani Sasu Akizungumza Katika Uzinduzi Huo
Aliyeshika "mic" ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto Dkt. Paschal Mbota Akizungumza Katika Uzinduzi Huo
Aliyeshika "mic" ni Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Wilaya ya Kiteto Dkt. Israel Akizungumza Katika Uzinduzi Huo
Aliyeshika "mic" ni Afisa Usafi na Mazingira Bw. Keveratus Sibanganya Akizungumza Katika Uzinduzi Huo
Aliyeshika "mic" ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Njoro Bi. Petrolina Mathayo Akizungumza Katika Uzinduzi Huo
-------------------------------------------- HANARI KAMILI --------------------------------------------
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Bw.Tamim Kambona kupitia mradi wa "P4R - Perfomance for Results - Lipa kwa Matokeo" amezindua kampaini ya usafi wa mazingira ikizingatia zoezi la ujenzi wa vyoo bora na matumizi ya vyoo. Uzinduzi huo umefanyika Kiwilaya leo tarehe 24.08.2020 Kata ya Njoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Bw.Tamimu Kambona.
Ujumbe maalumu katika uzinduzi huo ni "usichukulie poa nyumba ni choo", hivyo kila kaya inatakiwa kuwa na choo tofauti na ilivyo sasa. Mganga mkuu huyo wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Dkt.Pascal Mbota amesema "baadhi ya wananchi hawajaona umuhimu wa matumizi sahihi ya vyoo" lakini kinga ni bora kuliko tiba, suala la kuwa na choo bora na kuweka mazinga ya usafi basi afya pia itaimarika na hivyo utakuwa umejiweka katika mazingira salama ya kutougua mara kwa mara.
Katika uzinduzi huo mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw.Tamim Kambona Tamimu Kambona "amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa matumizi ya vyoo akidai madhara ni makubwa. Mgeni rasmi huyo aliendelea kusisitiza kwamba atahakikisha maeneo yote ya huduma za jamii yanakuwa na vyoo na kuwataka wananchi nao makazi yao yawe na vyoo kuepukana na madhara hayo.
Hata hivyo, Ofisi ya Mkurungezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imetoa zaidi ya Tshs. Milioni 86,400,000/= zitakazowezehsa ujenzi wa vyumba vya madarasa 4, ofisi ya waalimu 1 na vyoo Shule ya Msingi Njoro.Kimsingi hauwezi kuzalisha kama mazingira yanayokuzunguka ni hatarishi kwa afya yako hivyo kuweka hali ya usafi wa maeneo yetu inatupa fursa ya kutumia muda vyema kwenye shuguli za uzalishaji mali kwani kutaongeza ufanisi na tija ya uzalishaji na kuleta matokeo chanya si tu kwa kaya husika bali na kwa taifa kwa ujumla.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa