• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Awataka Watumishi Wilayani Kiteto Kuishi katika Maeneo Yao ya Kazi

Imetumwa : January 17th, 2018

                                          Mkuu wa Wilaya ya Kiteto  Mhe. Tumaini Magessa  Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti  Kuzungumza na wakazi wa Kata ya Njoro Katika  Mkutano wa Hadhara Uliofanyika Katika Kata hiyo Wilayani Kiteto.


                         Mbunge wa Jimbo la Kiteto  Mhe. Emmanuel Papiani akijitambulisha Katika Mkutano wa Hadhara Uliofanyika Katika Kata ya Njoro Wilayani Kiteto.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Awataka Watumishi  Wilayani  Kiteto Kuishi  katika Maeneo Yao  ya  Kazi


Mkuuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti amewataka watumishi wilayani Kiteto kuishi katika maeneo wanayofanyia kazi ili iwe rahisi kupatikana wakati wote wananchi wanapowahitaji.Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara  uliofanyika katika kijiji cha Njoro, kata ya Njoro wilayani Kiteto  kufuatia  malalamiko ya wananchi kuhusu watendaji wa vijiji pamoja na mtendaji wa kata  kuishi nje ya kata hiyo. 


Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Mnyeti amesema kwamba watumishi wanatakiwa kuishi katika maeneo wanayofanyia kazi,na kama mtu hawezi kufanya hivyo aache kazi. Katika kutaka kuthibitisha madai ya wananchi kuhusu watendaji hao , Mhe. Mnyeti aliwataka watumishi wote  wa serikali waliokuwepo katika mkutano huo kupita mbele na kila mmoja kueleza mahali anakoishi, na na hapo ikabainika kwamba watendaji wote wa vijiji pamoja na mtendaji kata  wanaishi Kibaya. Ndipo Mheshimiwa Mnyeti akatoa  agizo kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto  ndugu Tamim Kambona kuwahamisha watumishi wote ambao hawaishi katika kata hiyo. Mhe. Mnyeti anasema ‘‘Mkurugenzi hamisha watendaji wote hawa ambao hawaishi Njoro peleka katika vijiji na kata zilizoko mwisho wa mipaka kabisa ya wilaya hii”. Sambamba na agizo hilo, Mhe. Mnyeti ametoa kiasi cha shilingi za Kitanzania 1,000,000 kwa walimu , daktari na wauguzi wa zahanati ya Njoro ambao wanaishi katika  maeneo yao ya kazi.


Vilevile Mhe. Mnyeti ametoa agizo kwamba  mlima Simu uhifadhiwe kwa ukamilifu. Agizo hilo hilo la mheshimiwa Mnyeti limetokana na baadhi ya wakazi wa kata hiyo kuwasilisha kero zao kwake, ambapo kero kubwa  ni wakazi wa kijiji  cha Njoro  kunyang’anywa mashamba yao na kufanywa kuwa sehemu ya hifadhi, jambo ambalo linasababisha wao kukosa mashamba ya kulima hali ya yakuwa wao wanategemea kilimo kuendesha maisha yao . RC Myeti kwa kutaka kujua ukweli wa jambo hilo akawaagiza watu wote wenye mashamba katka mlima huo kupeleka  vithibitisho vyao ambavyo vinaonyesha kwamba wao ni wamiliki halali wa mashamba hayo ili wapatiwe mashamba mengine.Na hapa mheshimiwa Mnyeti anasema “ Watu wote wenye mashamba katka mlima wa simu pelekeni kwa mkuu wa wilaya vithibitisho vyenu vyote  vinaonyesha kwamba  ninyi ni wamiliki halali wa mashamba katika mlima huo. Ikithibitika pasipo shaka kwamba ninyi ni wamiliki halali, jiorodhesheni majina yenu mpeleke kwa mkuu wa Wilaya,mimi nitajua nitakako wapeleka kuwapatia mashamba.Nataka mlima huu uhifadhiwe kikamilifu kwa manufaa ya vizazi vijavyo,lakini pia sitaki kumuonea mtu’’.


Kero nyingine zilizowasilishwa na wananchi katika mkutano huo ni pamoja  na uchakavu wa majengo ya madarasa katika shule ya Msingi Njoro,migogoro ya mipaka,mgogoro  kati ya kata ya Njoro na Kata ya Partimbo  unaohusu umiliki wa eneo la mlima  ambalo lina minara ya  makampuni  ya simu ,mwenyekiti wa kijiji cha Njoro kutoonyesha ushirikiano pindi anapopewa taarifa za matatizo mbalimbali ya wakazi wa kijiji hicho na matibabu ya wazee ambapo mzee mmoja alimueleza mheshimiwa Mnyeti kwamba hawajapewa kadi za matibabu zinazotolewa kwa wazee jambo ambalo linawapa wakati mgumu pale wanapohitaji kutibiwa.


Mheshimiwa Mnyeti akatoa majibu ya kero hizo ambapo  katika kero ya uchakavu wa madarasa Mhe. Mnyeti amewataka wananchi kuchangia ujenzi wa majengo hayo ,na wakishaonyesha  nguvu zao  serikali itamalizia. Pia  amechangia shilingi 1,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa katika shule hiyo. Kadhalika  amemtaka afisa mipango wa Wilaya ya Kiteto (DPLO)  ndugu Beatrice Lumbeli kuwaelimisha wananchi  kuhusu kuibua miradi itakayopelekwa  katika vikao husika ili itakapopitishwa na kutekelezwa katika kata zao itokane na vipaumbele vyao  kuondoa malalamiko na kuwafanya wananchi hao kuithamini miradi hiyo. Katika hili Mheshimiwa myeti anasema “ waelimisheni hawa watu jinsi ya kuibua miradi.Afisa mipango tembelea vijiji vyote waelimishe wananchi’’.


Kuhusu  Migogoro ya mipaka, Mhe. Mnyeti ametoa rai kwa wananchi kuacha kuchochea migogoro hiyo, kwani mipaka hiyo imewekwa kwa sababu za kiutawala na haina athari kwa mwananchi yeyote  hivyo isiwe sababu ya wananchi kugombana. Pia amewaonya wanasiasa kutochochea migogoro ya mipaka kwa sababu zao za kisiasa .Mhe.Mnyeti anasema “ Acheni kufanya siasa kwenye maisha ya watu,nitawashughulikia”.


Katika kutatua mgogoro wa umiliki wa eneo lenye minara Mhe. Mnyeti  amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa kuipitia mikataba yote ili kujua   minara hiyo iko upande gani kati ya Njoro au Partimbo.Kuhusu mwenyekiti wa kijiji cha Njoro Mhe. Mnyeti  anasema “ mwenyekiti umelalamikiwa sana . Busara ni wewe mwenywe kujitathmini kama unatosha au la.Kama ukiona unatosha endelea,kama utaona hutoshi pisha’’. Kwa upande wa matibabu ya wazee  Mhe. Mnyeti alimtaka mganga mkuu wa Wilaya ya Kiteto Daktari  Malkiadi Mbota kujibu kero hiyo ambapo Dkt. Mbota amesema kwamba wazee kuanzia miaka 60 wanatibiwa bure,na katika utaratibu wa kuwatambua , mchakato ulishaanza ,na tayari jumla ya wazee 100 wa kata hiyo wameshapewa vitambulisho vya matibabu. Vilevile Mhe. Mnyeti amechangia kiasi cha  shilingi milioni moja kwa ajiri ya marekebisho ya zahanati ya Kijiji cha Njoro.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa