• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Awataka Wanavijiji Kiteto Kuheshimu Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi.

Imetumwa : January 17th, 2018



                             Wakazi wa Kata ya Kijungu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti Katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata ya Kijungu Wilayani Kiteto                                         


                                                                                                                  ................. HABARI KAMILI ..................


Mkuu wa Mkoa  wa Manyara  Awataka  Wanavijiji  Kiteto  Kuheshimu  Mipango ya Matumizi Bora ya  Ardhi.


Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti  amewataka wananchi wanaoishi vijijini kuheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi  waliyojiwekea katika vijiji vyao. Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara ulifanyika katika kata ya Kijungu ,wilayani Kiteto kufuatia kero zilizowasilishwa  na wananchi  katika mkutano huo wa hadhara ambapo kero kubwa ni migogoro inayohusu  wafugaji kuchungia kwenye  mashamba ya wakulima na kuweka makazi kwenye maeneo ya mashamba,wakulima kuanzisha mashamba katika maeneo ya malisho,pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali kutenga maeneo  ya hifadhi  bila utaratibu unaoeleweka na kusababisha baadhi ya wakulima kukosa maeneo ya kulima .


Akijibu kero hizo  Mhe. Mnyeti amesema kwamba matumizi bora ya  ardhi Katika vijijji yamepangwa na wanavijiji  wenyewe,lakini wanavijiji hao hao ndio hawataki kufuata matumizi hayo. Mahali popote ambapo wananchi wameweka mipango ya matumizi bora ya ardhi ,mipango hiyo iheshimiwe.Akitoa onyo kwa wanavijiji wanaotumia ardhi kinyume na mipango iliyowekwa Mhe. Mnyeti anasema “ Kuchungia kwenye mashamba ni kosa,kuvamia  maeneo ya malisho na kutengeneza mashamba ni kosa, watu waishi kwa kuheshimiana.Mkulima amheshimu mfugaji ,na mfugaji amheshimu mkulima.Tatizo kubwa ninaloliona katika wilaya hii ni matumizi  ya ardhi.Hili ni tatizo kubwa sana. Kama vijiji havikubaliani  na mipango  iliyopo sasa badilisheni. Mipango hiyo sio msahafu wala biblia , wanavijiji wakae  wabadilishe matumizi . Hata hivyo Mheshimiwa Mnyeti amewataka wanavijiji hao kufuata utaratibu katika kufanya mabadiliko hayo ambapo  anasema ‘‘ Mtu asibadilishe matumizi ya ardhi hadi vikao halali vikae vithibitishe mabadiliko hayo” Vilevile Mhe. Mnyeti amesema kwamba mabadiliko  ya matumizi ya ardhi yatakapokuwa yamekubalika watu wasibadilishe ili kuepusha migogoro. Sambamba na hayo Mhe. Mnyeti ametoa miezi mitatu kwa mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa kushirikana na wataalamu wa ardhi  wa halmashauri kukamilisha mchakato wa mabadiliko hayo.


Katika hatua nyingine Mhe. Mnyeti amewaagiza maafisa ugani  kufanya tathimini stahiki kila inapotokea uharibifu wa mazao unaosababishwa na wafugaji kuchungia katika mashamba, na wasimamie wahusika wa mashamba hayo kulipwa mara moja .Pia amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kiteto SP Fadhili Luoga Kuwakamata wafugaji wote wanaofanya hivyo  pamoja na ng’ombe zote zilizofanya uharibifu  na kutoza faini kwa kila ng'ombe mmoja ili kukomesha vitendo hivyo.


Wilaya ya  Kiteto imekuwa na migogoro ya ardhi  ya muda mrefu ,migogoro ambayo inahusisha wakulima na wafugaji ,pamoja na kwamba kuna mipango ya matumizi bora ya ardhi ambayo imewekwa  na vijiji vya wilaya hiyo ambapo mipango hiyo  inaainisha maeneo ya kilimo, maeneo ya malisho na maeneo ya makazi.


                                                                                                                                   ................ MWISHO......................


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa