• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Mkoa wa Manyara atoa Siku 14 Kupatikana Uongozi Mpya wa Hifadhi ya Msitu wa SULEDO Kiteto

Imetumwa : January 16th, 2018


                            

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akitoa maelekezo kuhusu SULEDO  katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika viwanya vya soko, kata ya Sunya - wilayani Kiteto



                   Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akitoa ufafanuzi kuhusu mwongozo wa SULEDO  katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika viwanya vya soko, kata ya Sunya - wilayani Kiteto



        Wakazi wa kata ya Sunya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti alipokuwa akizungumza nao katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika viwanya vya soko, kata ya Sunya.


                                                                                        ...................HABARI KAMILI..............


Mkuu wa Mkoa wa Manyara  atoa Siku 14 Kupatikana Uongozi Mpya wa Hifadhi ya Msitu wa SULEDO Kiteto


Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti  amemuagiza mkuu wa wilaya ya Kiteto  mheshimiwa Tumaini Magessa  kusimamia na kuhakikisha kwamba  hifadhi ya Msitu wa SULEDO inapata uongozi mpya ndani ya siku 14.Mhe. Mnyeti ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika  viwanja vya soko, kata ya Sunya wilayani Kiteto.


Agizo hilo la Mhe. Mnyeti limekuja baada ya wananchi wengi kulalamika juu ya ubadhilifu unaofanywa na viongozi wa hifadhi hiyo ,ambapo baadhi yao wamesema  kwamba  hawaelewi maana ya msitu huo wa SULEDO kwa sababu haunufaishi vijiji vinavyounda hifadhi hiyo,badala yake  unanufaisha watu wachache ambao ni viongozi wa hifadhi hiyo. Kwani mauzo yanayotokana na mazao ya Hifadhi hiyo hayajulikani yanakokwenda wala yanavyotumika. Vilevile  wananchi wa Sunya wamesema kwamba hawaelewi  mipaka halisi ya Msitu wa SULEDO  kwani wamekuwa wakiamriwa kuondoka kwenye mashamba yao wakiambiwa kwamba ni maeneo ya hifadhi  hali ya kuwa  wao ni wamiliki wa mashamba hayo kabla ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo. Kufuatia malalamiko ya wakazi wengi wa kata ya Sunya, Mheshimiwa Mnyeti anatoa agizo anasema ‘‘ malalamiko ya wananchi yanapokuwa mengi sana yanajenga chuki kati ya wananchi na serikali yao.Sasa mimi natoa agizo, mkuu wa wilaya nakupa siku 14  kushughulikia suala la SULEDO.Kuanzia sasa uongozi wa SULEDO  nimeuvunja .Halafu sasa kasimamie uongozi mpya upatikane ndani ya hizo siku 14”.


 Aidha Mhe. Mnyeti ameelekeza utaratibu utakaotumika katika kuchagua uongozi wa hifadhi hiyo  ambapo amemtaka Mkuu wa wilaya ya Kiteto  mheshimiwa Tumaini Magessa  kusimamia  mchakato wote wa upatikanaji wa uongozi huo mpya. Hapa Mhe. Mnyeti anasema‘‘.Nenda kasimamie  upatikanaji wa wajumbe watatu watatu kwenye kila kijiji.Nataka wewe ndio uende kwenye hiyo mikutano kwenye kila kijiji, uhakikishe akidi imetimia ,mwenyekiti yupo ,mtendaji wa kijiji yupo, wananchi wachague wenyewe kwamba sisi tunamwamini fulani  na fulani watuwakilishe kwenye SULEDO katika vijiji vyote 13”.


 Katika hatua nyingine Mhe. Mnyeti  pia amemtaka Mhe. Magessa   kuhakikisha kwamba baada ya kupatikana kwa uongozi mpya wa msitu huo , Afisa misitu na afisa wa  Wakala wa Huduma za Misitu ( TFS) wanatoa semina  kwa uongozi huo  kuwafundisha namna wanavyoweza kusimamia msitu wao,ili msitu huo uwanufaishe wananchi wote,kwani usipowanufaisha wote. Wananchi watauharibu. Akisisitiza juu ya umuhimu  wa hifadhi  hiyo kuwa na manufaa kwa wananchi wote, Mhe. Mnyeti anasema ‘‘Msitu huu usipowanufaisha wananchi wote,wataanza kuuharibu , na wakiuharibu serikali itawakamata, na ikiwakamata wananchi wanajenga chuki na serikali yao hali ya kuwa wataalamu wapo na watawala tupo”.


Msitu wa SULEDO ni msitu ambao  umeundwa na kata tatu za Sunya ,Lengatei na Dongo  ambapo wananchi toka vijiji 13 vya kata hizo walitoa ardhi ya vijiji vyao na kutenga kuwa msitu wa hifadhi ya jamii.

  

                                                                                   ............... MWISHO...............                


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUA: HATIMAYE KALOLENI YAPATA SHULE MPYA YA MSINGI

    July 30, 2025
  • SHULE YA MSINGI KINANGALI NAYO YANUFAIKA NA MRADI WA BOOST

    July 30, 2025
  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA YAENDELEA KUWEKEZA KWA VITENDO: KURASH YAPATA MRADI MWINGINE WA MILIONI 153 KUPITIA BOOST

    July 30, 2025
  • KATA YA BWAWANI YAPATA MRADI WA SHULE MPYA YA ELIMU MSINGI.

    July 28, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa