Habari picha ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema akiwa kwenye mkutano wa hadhara na wananchi katika Shule ya Msingi Orchaniodo siku ya Julai 23,2025.
Katika mkutano huo, Mhe. Mwema aliutambulisha mradi wa ujenzi wa madarasa mapya manne ya elimu msingi na vyoo matundu sita pamoja na madarasa ya mfano ya awali pamoja na vyoo matundu sita kwaajili ya wanafunzi wa awali. Gharama ya mradi huo ni 182,700,000.
Aidha wananchi hao pia walipata nafasi ya kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili na Mhe. Mwema aliahidi kuzifanyia kazi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa