Mkuu wa Wilaya ya Kiteto SSI Mbaraka Batenga Agosti 26,2023 amewaongoza wananchi wa mjini Kibaya katika zoezi la usafi wa Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika stendi ya mabasi mjini hapo.
Zoezi hilo lilihudhuliwa na watu mbalimbali akiwamo Katibu Tawala wa Wilaya Bi Mufandii Msaghaa, wafanyakazi kutoka Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza pamoja na wafanyakazi kutoka Halmashauri na taasisi mbalimbali ikiwamo TAKUKURU. Pia wananchi, wafanyabishara pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali walijumuika katika zoezi hilo.
Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Afisa Afya Mazingira (W) Bwana Lucas Magubika alisema “Ninatoa rai kwa wananchi kuendelea na usafi sio Jumamosi ya mwisho wa mwezi tu bali iwe tabia ili kujikinga na maradhi mbalimbali kama kuhara na kipindupindu”.
Serikali ilirasimisha Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa ni siku ya usafi Kitaifa kupitia sheria ya mazingira ya mwaka 2004 kifungu 191. Wilayani hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, CPA. Hawa A. Hassan amewapa majukumu maafisa watendaji kata kusimamia suala la usafi kwenye kata zao.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa