Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Mh. Lairumbe Mollel akifungua kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya wilaya ya Kiteto Mh. Hassan Benzi akichangia hoja katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Emmanuel Mwagala akijibu hoja za waheshimiwa madiwani katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Kikao cha baraza la madiwani kikiendelea katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Waheshimiwa mdiwani wakifuatilia kwa makini mijadala katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto
Wataalamu wa fani mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya kiteto wakijibu hoja za waheshimiwa madiwani katika baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto
HABARI KAMILI...
Mkuu wa wilaya ya Kiteto awataka madiwani kusimamia elimu katika kata zao
Mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magessa amewataka madiwani kusimamia elimu katika kata zao.Mkuu wa wilaya ameyasema hayo alipokuwa akitoa maelekezo ya serikali katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kiteto.Akizungumza katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, mkuu wa wilaya amesema kwamba suala la elimu limekuwa tata katika wilaya ya Kiteto ,na mpango mkakati uliopo ni kuongeza kiwango cha elimu na ufaulu , na kwamba kila diwani kwenye eneo lake la kazi apite kila mahali kujua kama walimu wake wanakwenda shule, na kama wanakwenda shule,wafuatilie kama wanafundisha inavyotakiwa. Mkuu wa wilaya amesema “Madiwani tufuatilie suala la elimu ili kujua tatizo liko wapi linalosababisha matokeo mabaya katika shule zetu.Tusipowasimamia walimu hatuwezi kuondoa tatizo la kushuka kwa elimu katika kata zetu.Tutafute njia ambazo tutatumia kuwabana walimu katika kata zetu ili wafanye kazi’’ .
Mkuu wa wilaya amesema kwamba katika wilaya ya Kiteto bado kuna vijiji ambavyo havina shule,vijiji hivyo ni Ngapapa na Leluku ,na kumuagiza diwani wa kata ya Kijungu mheshimiwa Mandalo Mussa kuhakikisha kwamba ifikapo tarehe 01 mwezi Novemba ujenzi wa madarasa katika vijiji hivyo unaanza kwa kutumia matofali yaliyopo ambayo yametolewa na wananchi wa vijiji hivyo,huku jitihada za haraka za kupata simenti na vifaa vingine zikiendelea kufanyika ili ujenzi huo uweze kuendelea na hatimaye madarasa hayo yaweze kukamilika ndani ya muda mfupi ili watoto wanaoishi katika vijiji hivyo waweze kwenda shule kwa urahisi, kwani kwa sasa shule ipo umbali wa kilometa kumi na saba (17) kutoka katika vijiji hivyo jambo ambalo linaweza kuwa sababu mojawapo ya matokeo mabaya na kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya ya Kiteto kwani katika hali ya kawaida sio rahisi mtoto kutembea KM 34 kila siku kwenda na kurudi shule ,watoto watakuwa wanaaga kwenda shule lakini hawafiki shule, wanafika shule wakati wa mitihani ,matokeo yake wanafanya vibaya na kusababisha kushuka kwa ufaulu katika wilaya.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ameelezea suala la pori la akiba la Mkungunero ambapo amesema kwamba suala la Mkungunero linahitaji historia na uelewa,mkuu wa wilaya alieleza historia ya mgawanyo wa maeneo uliosababisha mgogoro huo wa Mkungunero,na jitihada mbalimbali zilizofanyika katika kutatua mgogoro huo, na kwamba yeye kama mkuu wa wilaya amefanya jitihada binafsi ikiwemo kukutana na viongozi wa wilaya jirani ambazo ziko katika mgogoro kuhusiana na suala hio katika mikutano ya ujirani mwema,pia kukutana na waziri wa mali asili na utalii pamoja na uongozi mzima wa wizara hiyo, ambapo waziri wa mali asili amesema kwamba suala hilo lisifanyiwe maamuzi ya haraka ,hivyo baada ya kikao kati yake na uongozi wa wizara ya mali asili, iliamuliwa kwamba wizara zote tatu zinazohusiana na suala hilo (OR - TAMISEMI,wizara ya mali asili na utalii na wizara ya ardhi) zitakaa kujadili na kufikia maamuzi juu ya nini kifanyike kuhusiana na suala hilo.Baada ya maelezo hayo Mkuu wa wilaya amewataka madiwani kusubiri maelekezo ambayo yatatolewa mara baada ya wizara hizo kukaa .
Kadhalika mkuu wa wilaya amezungumza kuhusu zoezi la kupiga chapa ngo’mbe ambapo amesema kwamba kuna watu wanaeneza maneno ya upotoshaji kwamba ng'ombe zikipigwa chapa zitakaa miaka minne bila kuzaa ,hivyo amewataka madiwani wawaeleweshe wananchi wao umuhimu wa kupiga chapa ng’ombe.Mkuu wa wilaya amesema “Tunapotoka katika kikao hiki tuwe mabalozi wazuri kuhusu jambo hili.Tuwaeleweshe wananchi vizuri na kwa upole waelewe umuhimu wa zoezi hilo, ili lisikwame.
Mkuu wa wilaya pia amezungumza kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta, ambapo litapita katika wilaya ya Kiteto, amesema kwamba ujenzi wa bomba la mafuta upo katika mchakato ,makampuni mbalimbali yanafika wilayani kiteto kwa ajili ya kufuatilia mambo mbalimbali kuhusiana na ujenzi wa bomba hilo .Makampuni hayo yapewe ushirikiano unaostahili ili kuunga mkono agizo la mheshimiwa Rais.
Aidha shughuli za kawaida za baraza ziliendelea kulingana na ajenda zilizokuwepo ambapo taaarifa za miradi ya maendeleo kwa kwa kila kata ziliwasilishwa na kupokelewa ambapo madiwani walieleza hatua ilipofika, miradi hiyo ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, mabweni , zahanati na uhifadhi na usimamizi wa mazingira ya mlima simu.Katika kuwasilisha taarifa hizo za miradi ya maendeleo, madiwani walielezea masikitiko yao ambapo wamesema kwamba kumekuwepo na tatizo ambalo ni serikali kutokuleta fedha za miradi,tatizo ambalo linasababisha miradi mingi kukaa muda mrefu bila kukamilika pamoja na jitihada za wananchi kuanzisha miradi hiyo na kuchangia gharama .
Pia madiwani waliwasilisha majina ya wajumbe wa mabaraza ya kata ,ambapo majina hayo yalipokelewa .Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto mheshimiwa Lairumbe Mollel aliwataka madiwani ambao hawajawasilisha majina hayo kuhakikisha kwamba wanawasilisha kabla ya kikao cha kamati ya fedha na mipango,ili yaweze kujadiliwa na kupitishwa katika kikao hicho ili wajumbe hao waweze kupatiwa mafunzo na hatimae mabaraza hayo yaweze kuanza kutekeleza majukumu yake mapema iwezekanavyo.
Katika kikao hicho pia baadhi ya madiwani walizungumzia tatizo la kuwepo kwa popo katika majengo ya serikali ,ambapo popo hao wamekuwa wakiharibu paa za majengo ,ilhali baadhi ya majengo hayo yakiwa bado ni mapya ,lakini huharibiwa na popo hao.Kutokana na kuwasilishwa kwa tatizo hilo la popo, madiwani hao walishauriwa kutumia bati nyeupe za plastiki kupaua majengo katika maneo ambayo yameonekana kuwa na tatizo hilo la popo,kwani bati hizo huingiza mwanga,ambapo hali ya kuwepo kwa mwanga katika majengo hayo hufanya popo hao kuondoka.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa