Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa Akikagua Mazoezi Hayo Katika Viwanja vya Michezo Kiteto Sekondari
Watumishi Mbalimbali na Wanafunzi Wakijiachia Vilivyo na Mazoezi ya Viungo Kama Inavyoonekana Hapo Juu.Askari Mmojawapo Akitembea Juu ya Tumbo la Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibaya Afande Partrick Kimaro Maarufu "Sabasita" Kwa Kuonyesha Ukakamavu wa Hali ya Juu Alionao.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa Akitembea Juu ya Tumbo la Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibaya Afande Partrick Kimaro Maarufu "Sabasita" Kwa Kuonyesha Ukakamavu wa Hali ya Juu.
Watumishi Wakirudi Toka Mazoezini
----------------------------------------------- HABARI KAMILI -----------------------------------------------
Wakati zoezi la usafi wa Kitaifa likiendelea kwa wananchi, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa amesisitiza watumishi wote wa Serikali kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kuimarisha afya zao. Maneno haya ameyasema leo asubuhi katika viwanja vya michezo shule ya Kiteto sekondari Mjini Kibaya Wilayani Kiteto. Awali mazoezi haya yalihusisha watumishi wa serikali zikikiwemo Taasisi mbalimbali za serikali kama vile Polisi, Magereza, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na wanafunzi toka shule za bwneni za jirani kama vile Kibaya Sekondari, Bwakalo Sekondari na Kiteto Sekondari.
Mazoezi haya yalianza saa 12:00 asubuhi katika Kituo cha Polisi Kibaya Mjini kwa kukimbia mbio za kawaida hadi viwanja vya michezo vya Kiteto sekondari ambako kule mambo yalikuwa mazuri sana na kila mshiriki amefuraha sana ufanisi wa mazoezi haya yaliyodumu kwa muda wa masaa mawili na nusu.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa amesema ni muhimu kama mtu kajafanya mazoezi mazito kama haya basi ahakikishe anarudia tena kwa siku mbili tatu mfululizo ili kuuweka mwili sawa kwani bila kufanya hivyo mwili utakuwa na uchovu mwingi zaidi na hata kuugua viungo.
Watumishi wote wanaofika katika mazoezi haya wanashauriwa kuwa na mavazi ya staha na ya kimazoezi pia mfano kwa wanawake na wasichana ni muhimu kuvaa "track suit" na kiatu kinachoendana na raba lakini sketi ni nzuri kuvaa ila ni lazima mhuhusika aongeze na uvaaji wa suluari ndani au "track sout" na sio nguo nyepesi kama "skin tight"
Wakiongozwa na wabobezi wa mazoezi haya yaani askari Polisi toka Kituo cha Polisi Kibaya na Kiongozi wao Mkuu wa Kituo Afande Patrick Kimaro maarufu kama "Sabasita"
Baada ya kufunga mazoezi haya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa amesema tutaendelea na mazoezi haya Jumamosi ya wiki ijayo tarehe 02.10.2019 kwa kufuata muda ule ule wa saa 12:0 asubuhi na mahali pa kukutana ni pale pale Polisi Kituoni Kibaya.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa