Mkuu wa wilaya ya Kiteto, Mh. Mbaraka Al Haji Batenga akizungumza kwenye kikao cha maendeleo ya Wilaya (DCC) tarehe 14/12/2021, aliwaagiza Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata na Vijiji watatue migogoro ya ardhi katika maeneo yao kabla ya shughuli za kilimo kuanza rasmi. Pia alisema kuwa migogoro mingi Wilayani Kiteto inasababishwa na baadhi ya viongozi wa vijiji kutokuwa waadilifu na kuifanya kuwa vyanzo vya mapato yao na kusema kamwe hatolifumbia macho, kiongozi yeyote atakaye husika sheria itafuata mkondo wake.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Bw. John Nchimbi aliwataka watendaji wote wafanye kazi kwa weledi ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima katika maeneo yao na alisema ataanza kuwashughulikia maafisa watendaji wa kata na vijiji watakaokuwa vyanzo vya migogoro hiyo akisema, “kipimo cha mtumishi kama anawajibika ni pamoja na uwepo wa amani katika eneo lake”.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa