Meza Kuu Katikati ni Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa Akiwa na (kulia kwake) Afisa Michezo (W) Bi. Juliana Mtei, Afisa Utamaduni (W) Bi. Hawa Masawika na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kiteto Bw. Peter Nyigu Wote Wakiangalia Mechi za Shirikisho la Kombe la Azam Tanzania kwa Mwaka 2019/2020 Zilizofanyika Katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Wilaya ya Kiteto.
Kushoto ni Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Mhandisi Tumaini Magessa Akipokelewa na Mwenyeji wake Bw. Hamadi Muya Katibu Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kiteto.
Wadau Wakubwa wa Shirikisho la Kombe la Azam kwa Wilaya ya Kiteto Benki ya CRDB Tawi la Kibaya "Ulipo Tupo" Nao Walijumuika na Mashabiki wa Timu Zote Mbili Uwanjani Hapa Kutoka Kushoto ni Joseph Kisipa, Edwin Swai, Lucy John na Diclan Assey.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB Tawi la Kibaya "Ulipo Tupo" Kutoka Kushoto ni Edwin Swai, Joseph Kisipa, Peter Nyigu ( Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kiteto), Lucy John (Meneja Benki ya CRDB Kibaya) na Diclan Assey.
Kamisa Bw. Haruna Kombo
Wachezaji wa Timu ya Red Star FC (Watumishi FC) ya Kiteto Wakifanya Mazoezi ya Viungo Muda Mfupi Kabla ya Kuanza Mpira.
Wachezaji wa Timu ya Royal FC ya Arusha Wakifanya Mazoezi ya Viungo Muda Mfupi Kabla ya Kuanza Mpira.
Wachezaji wa Timu Zote Mbili Wakipeana Salama za Kheri Tayari kwa Kuanza Mechi hiyo
Kutoka Kushoto Mwenye Jezi Nyekundu ni Nahodha wa Timu ya Red Star FC Bw. Abdullaziz Kibwana Wakipeana Mkono na Nahodha wa Timu ya Red Star FC (Watumishi FC) ya Kiteto Mwenye Jezi Nyeupe Kulia.
Watatu Kutoka Kushoto ni Mwamuzi (Refa) Mwenye Jezi Nyeusi na Mistali na Anayefuata Ni Haruna Kombo Kamisaa wakiwa na Manahodha wa Timu Zote Mbili na "Lines Men"
Timu ya Red Star FC ya Kiteto Muda Mfupi Kabla ya Kuanza Mechi Hiyo.
Hapo juu Mechi Inaendelea.
Timu Zote Mbili Zikienda Kwenye Mapumziko Baada ya Kipindi cha Kwanza Kuisha.
Hawa Ni Baadhi ya Watazamaji Waliofika Uwanjani Hapo.
Watoa Huduma Mbalimbali Walitumia Fursa Vizuri Katika Kujiongezea Kipato Kama Unavyoona Mpenzi Msomaji.
Huu ni Usafiri Uliotumiwa na Timu ya Royal FC Kutoka Arusha Kuja Kiteto.
------------------------------------------------------------- HABARI KAMILI -------------------------------------------------------------
Mashindano haya ni ya Mechi za Shirikisho la Kombe la Azam Tanzania kwa Mwaka 2019/2020 ambapo kwa sasa ni hatua za awali za mtoano.
Kabla ya mechi kuanza kulikuwa na mvua kubwa iliyoanza kunyesha muda wa saa nane alasili na kufanya uwanja mzima kuwa na utelezi mwingi lakini baada ya kipenga kulia na Mwamuzi Christopher Kamula saa 10:13 jioni mpambano ulianza kwa mahasimu hao kila mmoja kuusoma mchezo wa mwenzake.
Katika mechi ya leo kila timu ilihitaji kuendelea na mashindano haya kwa kumfunga mpinzani wake, hata hivyo katika kipindi cha kwanza mchezazi machachari wa Royal FC Joseph Mpeka aliipatia bao la kwanza timu yake ambalo lilidumu hadi kipindi cha mapumziko, timu ya Red Star FC (Watumishi FC) ya Kiteto iliongeza nguvu kwa kubadilisha wachezaji wake, kujituma zaidi na kuongeza kasi ya uchezaji uwanjani ili kurudisha majibu kwa mashambulizi makali ya goli la Royal FC lakini wapi hali ilikuwa ngumu hadi kipindi cha kwanza kilipoisha.
Kwa ujumla mashabiki wengi mno waliojitokeza kuishangilia timu ya Kiteto yaani Red Star FC (Watumishi FC) walikuwa na shauku kubwa kuona timu yao inashinda haikuwa hivyo, kwani baada ya mapumziko kipindi cha pili timu ya Red Star FC (Watumishi FC) ya Kiteto ilipachikwa bao lingine la pili na mchezaji yule yule Joseph Mpeka, lililodumu hadi kufikia mwisho wa mchezo Royal FC 2 na Red Star FC (Watumishi FC) 0. Kwa matokeo haya Red Star imeaga rasmi mashindano haya na Royal FC ya Arusha inaendelea na mechi zijazo.
Benki ya CRDB Tawi la Kibaya, "Ulipo tupo" hawakuwa nyuma kwani walishiriki ipasavyo katika kuhakikisha mechi hizi za Shirikisho la Kombe la Azam Tanzania kwa Mwaka 2019/2020 Wilayani Kiteto Mkoani Manyara wanapata huduma mbalimbali ili kufanikisha mechi hii.
Kwa upande mwingine kuwepo mara kwa mara kwa mechi kama hizi hususani za kutoka nje ya Wilaya huvutia watu wengi sana kushiriki kunakopelekea kuibuka kwa fursa mbalimbali za muda mfupi kwa wafanyabiarana na wajasilia mali kama vile nyumba za kulala wageni (Lodges & Guests), Usafirishaji "bodaboda, Taxis na daladala" Huduma za chakula na zingine pia hali hii huongeza mzunguko wa kifedha kwa eneo husika kupitia uwepo wa michezo hii.
Wakiongea kwa muda tofauti, wamesema tunawashukuru wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine ili kufanikisha michezo hii na wawe tayari kwa mashindano mbalimbali yanayofuata huko mbele.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa