Aliyesimama ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiteto Bw. Tamim H. Kambona ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Akifungua Mafunzo hayo Katika Maktaba ya Wilaya ya Kiteto Mjini Kibaya.
Aliyesimama ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kiteto Bw. Tamim H. Kambona ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Kutoka Kushoto ni Bi. Nakaji Mollel ni Kaimu Afisa Ugavi Wilaya ya Kiteto, Bw. Zabloni Lulandala Afisa Utumishi na Utawala wa Wilaya ya Kiteto
na Bi. Hdija Boffu Mtunza Hazina wa Wilaya ya Kiteto. Kutoka Kulia ni Bw. Zabloni Ndosi Mwanasheria wa Wilaya ya Kiteto na Bw. Lauenti Kimaro ambaye ni Afisa Uchaguzi Wilaya ya Kiteto.
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto Mh. Mwakyoma Katika Akiwa Katika Zoezi la Kuwaapisha Wasimamizi Hao.
Wasimamizi Hao Wakila Kiapo Mbele ya Hakimu wa Wilaya
---------------------------- HABARI KAMILI ----------------------------
Mafunzo haya elekezi yameanza leo tarehe 07.08.2020 hadi tehehe 09.08.2020 katika Maktaba ya Wilaya ya Kiteto. Hata hivyo ajira ya hawa watu inaanzia tarehe 05.08.2020 hadi tarehe 03.11.2020
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 74 kifungu cha 6 tume imepewa jukumu la kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Madiwani kwa Tanzania bara. Hawa ni wasimamizi ngazi ya kata lakini bado watendaji wengine wa vituo watateuliwa siku za mbeleni.
Msimazi huyo wa uchaguzi jimbo la kiteto aliendelea kwa kusema " ndugu washuriki uchaguzi ni mchakato unaoshirikisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatia kwa mujibu wa katiba sheria, kanuni na maelekezo ya tume. Taratibu hizo ambazo mtakazo elekezwa kwenye mafunzo ndiyo msingi wa uchaguzi kwa kuwa mzuri na wenye uhalisi, hivyo kwa kuzingatia na kutekeleza taratibu hizo kutapunguza kama siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi"
Hata hivyo msimamizi huyu wa jimbo la Kiteto amewaasa wasimamizi wasaidizi hawa wakumbuke hii kazi ya uchaguzi ni muhimu na itakuwa inaangaliwa na watu tofauti tofauti kwa hiyo wafanye kazi hii kwa uadilifu na kwa weledi wa hali ya juu.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa