Julai 17, 2024, Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto iliupokea Mwenge wa Uhuru na kukimbizwa umbali wa kilomita 68 wilayani hapo.
Ukiwa Wilayani hapa Mwenge wa Uhuru umezindua, kufungua na kutembelea miradi yenye jumla ya thamani ya TZS. Bilioni 3.37.
Katika mbio hizo, Mwenge wa Uhuru umefungua miradi miwili ambayo ni Majengo Matatu Mapya katika Hospitali ya Wilaya yenye thamani ya zaidi ya TZS milioni 900 na pia kufungua vyumba vitano vya madarasa pamoja na matundu nane ya vyoo katika shule ya Sekondari Kiteto mradi ambao una thamani ya zaidi ya TZS. milioni 139.
Aidha Mwenge wa Uhuru umezindua Daraja la Mawe la Mbeli lenye thamani ya zaidi ya TZS Milioni 400 pamoja kuzindua Mradi wa Maji Bwagamoyo wenye thamani ya zaidi ya TZS. Milioni 422.
Mbali na hayo Mwenge wa Uhuru umekagua shughuli 10 mbalimbali ikiwemo uwezeshaji wa wananchi kiuchumi pamoja na maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa