Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema Emmanuel leo Julai 13,2025 ameupokea Mwenge wa Uhuru 2025 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhe. Fakii Lulandala katika uwanja wa Sekondari ya Ndedo uliopo kata ya Ndedo.
Ukiwa wilayani Kiteto, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa umbali wa kilometa 171 na kutembelea miradi yenye thamani ya zaidi bilioni 1.4.
Ukiwa wilayani hapa, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kutembelea miradi saba ambapo miradi mitatu itazinduliwa, mitatu itatembelewa na mradi mmoja utawekewa jiwe la msingi.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 inasema "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu"
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa