Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Mhe. Abdala Bundala, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, CPA Hawa Abdul Hassan, kwa usimamizi bora wa ukusanyaji wa mapato.
Pongezi hizo zimetolewa Desemba 13,2024 kwenye kikao cha Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango baada ya kusomwa kwa taarifa ya mapato ambayo imeonesha kuwa hadi kufikia Novemba 30, 2024, Halmashauri tayari imekusanya robo tatu (75%) ya mapato yanayotarajiwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Mhe. Bundala pia aliwapongeza wataalamu wa Halmashauri na wananchi kwa ushirikiano wao uliofanikisha mafanikio hayo. Halmashauri ya Kiteto inalenga kukusanya jumla ya shilingi bilioni 3.9 katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Mafanikio haya ni ishara ya uwajibikaji na mshikamano wa wadau wote katika kufanikisha maendeleo ya Wilaya ya Kiteto.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa