Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Kiteto (aliyesiamama) Mh. L. Mollel akimkaribisha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Mh. Abdallah Ulega Kwenye Baraza la Madiwani Liliokuwa Likiendelea Katika Ukumbi wa Halmashauri Wilaya Kiteto, Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw.Tamim Kambona, Kuanzia Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kiteto Mh. Emanuel Papian anayefuta ni Mh. Hassan Benzi Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
--------------------------------- HABARI KAMILI ---------------------------------
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Mhe. Abdallah Ulega amepongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mh. Eng. Tumaini Magessa ambayeni ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto na Bw. Tamim Kambona ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji. Kiteto inafahamika kuwa ni ya wakulima wakubwa, wadogo na wakati vivyo hivyo Kiteto ni ya wafugaji wakubwa, wakati na wadogo kwa sasa migogoro haijaisha lakini uongozi umejitahidi sana kuipunguza ili isilete athari kwa wananchiNaibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Mhe. Abdallah Ulega amewasihi sana viongozi kuendelea na kasi ile ile ya kuimarisha amani kwa Halmashauri na kuhakikisha kila mgogoro wowote unaochipukia basi uwaiwe mapema kabla haujaleta madhara kwa wananchi.Hata hivyo Naibu Waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameelezwa kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto inatumia fedha nyingi katika migogoro hii ili kulinda amani ya Wilaya kitu ambacho kinapunguza kasi ya Halmashauri kujielekeza katika masuala ya maendelea kwa wananchi ikiwapo elimu, afya, barabara na maji, hii kwa kiwango fulani inafanya sisi kama Halmashauri tusifikie malengo mbalimbali ya kuwasaidia wananchi katika sekta tajwa hapo juu kwani fedha hizo hizo ndizo zinazotumika kugharamia zoezi la ulinzi na usalama wa eneo letu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega (aliyesimama) katika kuhakikisha tunafuata maagizo ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt J.P. Magufuli mambo matatu ni ya msingi kuyatekeleza ili kumuwezesha mjasiriamali yeyote kufikia malengo yake na kuinua uchumi wake na wataifa kwa ujumla hadi kufikia uchumi wa kati kwa mwaka 2025. Suala la kwanza inatakiwa eneo husika la mfugaji litambulike, kisha lipimwe na mwisho limilikishwe kwa muhusika.Hata hivyo Serikali ya Mh. Rais John P. Magufuli italeta tena dawa ya ruzuku kwa majosho yote yanayofanya kazi katika Halmashauri ya Wialaya ya Kiteto hii ni katika kuhakikisha Taifa letu linajitegemea kwa Uchumi na Teknolojia, ambapo hadi sasa tayari Serikali imeweza kutengeneza kwa mara ya kwanza chanjo sita (6) za mifugo ikiwemo ya ugonjwa wa mifugo wa Mdondo, Homa ya Mapafu, Ugonjwa wa Kutupa Mimba, Ugonjwa wa Chambavu na mengineyo, yote haya yamefanyika katika maabara zetu za hapa nchini Tanzania.
Lengo mahususi la Serikali ya Awamu ya Tano ni kutokomeza magojwa yote kwa wafugaji nchini ili kutanua wigo wa upatikanaji wa soko la uhakika katika nchi za nje hii itapelekea kukuza uchumi wa nchi yetu na wananchi wake kwa pamoja kwa kujenga fursa mbalimbali zitakazojitokeza kutokana na kupatikana kwa soko la kimataifa kama vile kuongeza ajira nchini, kuongeza kipato na kupata utajiri kwa wananchi wetu.
kimsingi Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega alifurahi sana baada ya kuona kuna ushirika wa maziwa hapa Kiteto akisema ni mwanzo mzuri sana kwani maziwa ya Tanga Fresh yanamilikiwa na ushirika wa maziwa wa wananchi wa Jiji la Tanga kilichobaki kwa sisi ni kusikiliza changamoto zao na kuwashika mkono pale wanapokwama ili wapate utajiri kupitia jasho lao.
Picha za Hapo juu ni Madiwani (waliovaa majoho mekundu) wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na Majoho ya Bluu ni Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri na Wataalamu Wengine wa Halmashauri Wakimsikiliza Naibu Waziri Mh. Abdallah Ulega.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa