Kutoka Kushoto Mwenye Koti ni Mzee Marandu Muwekezaji wa Mifugo Wilayani Kiteto
Kulia aliyesimama ni Katibu Tawala Wilaya ya Kiteto Bw. S. Ndaki akiwasilisha taarifa ya Wilaya ya Kiteto kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya wa Kiteto kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb), Mh. Abdallah Ulega katika Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kiteto na Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb), Mh. Abdallah Ulega baada ya kupokea taarifa ya Wilaya, kisha alizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kiteto na Baadhi ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto katika Ofisi ya Katibu Tawala Kiteto.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb), Mh. Abdallah Ulega Akizungumza Alipotembelea Eneo la Uwekezaji wa Mifugo la Bw. Marandu Wilayani Kiteto
Hao Hapo Juu ni Ng'ombe wa Bw. Marandu Wakiwa Katika Malisho Wilayani Kiteto
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb), Mh. Abdallah Ulega (aliyevaa shati la lenye maua) Akizungumza Alipotembelea Eneo la Uwekezaji wa Mifugo wa Wawekezaji Mbalimbali wa Sekta ya Mifugo Wilayani Kiteto
Mbunge wa Jimbo la Kiteto Akisisitiza Jambo Katika Maeneo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb), Mh. Abdallah Ulega Alipotembelea na Kuona Kero Mbalimbali Kwenye Maeneo ya Uwekezaji wa Sekta ya Mifugo Wilayani Kiteto
----------------------------- HABARI KAMILI ----------------------------
Bw. Laurenti Marandu ni Njasiriamali ambaye amewekeza kwenye ufugaji, ni mzaliwa wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyefika hapa Wilayani Kiteto mwaka 1990. Hadi sasa Bw. Marandu ana ng'ombe zipatazo 120 na ekari 200 nusu anazitumia kwa shuguli za kilimo kama vile kulima mazao aina ya mahindi, alizeti na mtama na zingine kwa shuguli za ufugaji ambapo ni ng'ombe wa maziwa na ng'ombe wa kunenepesha kwa ajiri ya nyama. Mzee Marandu alianza kazi ya ufugaji miaka 10 iliyopita ambapo hadi sasa lengo lake kuu ni kuwa na mradi mkubwa wa kunenepesha ng'ombe na kuuuza lakini hadi sasa hajaweza kufikia lengo hilo kutokana na changamoto mbalimbali.
Changamoto alizonazo ni kutokuwepo kwa maji ya kutosha ambapo hutumia visima vya kupampu kwa mkono kiasi kwamba hata akitaka kuotesha majani mengi ya malisho inashindikana na pia hakuna nishati ya uhakika kwa ajili ya kuweka mitambo mbalimbali ya kuwezesha miundombinu ya kisasa katika ene lake la uzalishaji.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega baada ya kuona haya alikubali kumpa mbegu ya ng'ombe dume bora aina ya Borani kutoka Ranch za taifa ili kumuongezea uwezo wa kufikia lengo la kuwa na ng'ombe wa nyama wenye uzito zaidi ya kilogramu 1000 kwa ng'ombe mmoja, pia Mh.Waziri aliongeza kuwa ataleta wataalamu kufika katika eneo hilo na kufanya tathmini mbalimbali za uboreshaji wa ufugaji wake ili atimize lengo lake la kuwa tajiri kupitia mifugo yake.
kuhusiana na Bwawa la maji Mh. Naibu Waziri Ulega amesema tumieni wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kutathmini na kuandika andiko litakaloanisha gharama za eneo la kupanua njia za kupitishia mifugo kuja kunywa katika bwawa hilo, gharama za namna ya kunyanyua matuta yatakayokuwa ni kingo za pembezoni na kutoa tope kwenye bwawa husika ili liweze kuhifadhi maji hali itakayosaidia maji kwa ajili ya mifugo na maji kwa ajiri ya kilimo cha umwagiliaji hususani mbogamboga na matunda kama matikiti.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa