• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

''Nataka Watu Waje Wajifunze Kiteto '' Naibu Waziri Waitara

Imetumwa : December 15th, 2018

Naibu waziri wa Or -TAMISEMI  Mhe. Mwita M. Waitara akitoa maelekezo kuhusu ujenzi wa jengo jipya la ofisi za halmashauri ya wilaya ya Kiteto , wakati wa ziara yake wilayani Kiteto mapema leo.


............. HABARI KAMILI ...........




Naibu waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mheshimiwa Mwita M. Waitara amesema kwamba kwa muda mfupi aliofanya ziara katika wilaya ya Kiteto ameona mambo mazuri ambayo anataka watu waje wajifunze .Mheshimiwa Waitara ameyasema hayo leo tarehe 15.12.2018 wakati wa ziara yake  katika wilaya ya Kiteto , mkoani Manyara .


Akizungumza mara baada ya kukagua  miradi ya ujenzi katika shule za Sekondari  za Kiteto  na Engusero pamoja na shule ya msingi Twanga Mhe. Waitara amesema “Kwenye awamu hii kwenda mpaka Januari kuna fedha zitakuja, nimeona tayari zimeshatengwa  kwa ajili ya ujenzi na madarasa na matundu ya vyoo kwa shule za msingi Kijungu,Makame na Mbikasi.Kwa mtindo ambao nimeuona hapa, naamini kwamba nyie Kiteto mtapata madarasa zaidi ya haya.Na ikiwezekana mzidishe usimamizi.Na sisi tutajitahidi tusukume ili fedha hizi zije , tuje tuangalie.Nitataka watu wafuate mtindo wenu, hii inaweza ikapunguza mzigo kwa serikali.Kwa sababu mahali pengine watu wanapewa 6,600,000/= wanajenga matundu sita ya vyoo wanakaa wanatulia, lakini nyie badala ya matundu sita mmejenga matundu 12 , badala ya madarasa matatu, mmejenga madarasa manne na ofisi  na kwa fedha hizohizo mmetengeneza madawati 60.Ni lazima watu waje wajifunze kwa nini hapa imewezekana, na wao kwa nini wanashindwa’’.


Mheshimiwa Waitara amesema kwamba changamoto kubwa ambayo wao kama serikali wanayo ni matumizi ya fedha, na kwamba changamoto hiyo  inatokana na watu kutumia fedha za serikali vibaya, watu kutojiongeza, ambapo  wamekuwa wakiishia kutekeleza miradi kwa idadi ileile waliyopangiwa ,hata kama fedha hizo  zingeweza kutosha kufanya zaidi ya idadi hiyo. Kitu ambacho kwa Kiteto imekuwa tofauti kwamba  wamefuata maelekezo ya serikali, lakini pia wameweza  kuongeza majengo na samani kwa kutumia kiasi hichohicho cha fedha,  na zaidi ya yote   wamezingatia viwango vya ubora katika ujenzi  .


Mheshimiwa Waitara pia ameipongeza Halmashauri kwa kutumia fedha za ndani kwenye miradi mbalimbali, kama vile ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari ya Kiteto ,bweni ambalo limeshapauliwa, na ujenzi wa bwalo ,ambalo liko katika hatua ya lenta na kuongeza fedha kiasi cha shilingi 20,000,000/= katika umaliziaji wa mabweni na ununuzi wa vitanda katika shule ya sekondari ya Engusero  pamoja na miradi mingine mingi katika sekta ya elimu na afya.Kadhalika mheshimiwa Waitara amewapongeza  wakazi wa kiteto kwa uchangiaji mzuri wa miradi ya maendeleo sambamba na usimamizi mzuri wa miradi, jambo ambalo limewawezesha  kutekeleza miradi mingi  katika ubora. Aidha Mhe. Waziri amesema kwamba ameyapokea na ameahidi kuyafanyia kazi  maombi yote yaliyowasilishwa  wakati wa ziara yake  .


Katika ziara yake hiyo ya siku moja Mhe Naibu waziri Waitara ametembelea maeneo mbalimbali kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo.Maeneo hayo ni Jengo jipya la ofisi za halmashauri, shule ya msingi Twanga, Shule ya sekondari Engusero na shule ya sekondari ya Kiteto,ambako pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa bweni ,pia ameweka jiwe la msingi katika bweni hilo.



..........MWISHO...........

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa