Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Ismail Ali Ussi, amewapa pole wananchi wa kata ya Partimbo kwa magumu waliyopitia wakati wa kuvuka korongo la Barabara ya Kibaya- Mbeli kabla ya kujengwa kwa daraja kubwa la mawe la midomo saba katika eneo hilo.
Pole hizo zimetolewa Julai 13,2025 wakati wa uzinduzi wa daraja hilo la mawe katika eneo hilo.
Akizungumza katika eneo hilo, kiongozi huyo alisema kwamba wananchi wa eneo hilo wameonesha uvumilivu, upendo, heshima na uzalendo wa hali ya juu.
"Yamefanyika mabadiliko makubwa ya kimaendeleo katika eneo hili. Nilipoona njia mliyokua mnapita mwanzo nilipata mshtuko wa hali ya juu, poleni kwa mliyoyapitia", ameongeza Ndg. Ismail.
Ujenzi wa daraja hilo la mawe umegharimu kiasi cha TZS 405 na kukamilika kwa dafaja hilo kunategemewa kuimarisha usalama wakati wa uvukaji wa eneo hilo msimu wa mvua na kuboresha mazingira ya usafiri na usafirishaji.
Aidha, kiongozi huyo aliwapongeza wananchi wa eneo hilo kwa kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa