Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim H. Kambona na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto Bw. Christopher Simwimba
Hatua za Awali za Ujenzi wa Kitalu Nyumba
Hatua za Awali za Utandazaji wa Bomba za Umwagiliaji Ndani ya Kitalu Nyumba HichoKutoka Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim H. Kambona Akimsikiliza Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Rodrick Kidenya Katika Kutoa Maelezo Ya Vijana Wanaoshugulikia Kitalu Nyumba Hiki na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto Bw. Christopher Simwimba
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bw. Tamim H. Kambona Akikagua Utekelezaji wa Mradi Huo na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto Bw. Christopher Simwimba
Bw. Emmanuel Magubika Akipogolea Nyanya Husika Ili Ziwe na Afya Zaidi
Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto Bw. Christopher Simwimba Akiwa Katika Ukaguzi wa Kitalu Nyumba Hicho
Afisa Kilimo na Umwagiliaji Bw. Balabala Pundungu Ambaye ni Mratibu wa Kitalu Nyumba Hicho
Bw. Ezra Mariki Akinyunyizia Mbolea Katika Miche Hiyo ya Nyanya Kwa Ustadi na Teknolojia ya Kisasa na Kimamboleo
Muonekano wa Nje wa Kitalu Nyumba Hicho na Miundombinu Mahususi ya Umwagiliaji Maji
------------------------------------ HABARI KAMILI -----------------------------------
Vijana wapatao zaidi ya 100 toka katika kata 4 za Partimbo, Bwagamoyo, Kibaya na Kaloleni wamenufaika na mradi wa Kitalu nyumba Wilayani Kiteto Mkoani Manyara baada ya kupata mafunzo elekezi ya siku 6 ya uzalishaji wa mimea aina ya nyanya kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba mwezi Agosti 2020. Mafunzo hayo yalifadhiliwa na ofisi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu na kusimamiwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya chini ya wataalamu wake wa Idara ya Kilimo umwagiliaji na Ushirika kwa kushirikiana na idara ya maendeleo ya jamii ambayo ndiyo yenye vikundi hivi vya vijana.
Kimsingi kampuni ya “Royal Agricultural Company Limited” ya Mkoani Morogoro ndiyo iliyopewa kazi hii na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutekeleza hili ileta vifaa, ilitoa mafunzo ya ujenzi wa kitalu nyumba na mafunzo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba kwa vijana 100; Wataalamu wa Kilimo na wataalamu wa Idara ya maendeleo ya jamii walikuwa ni miongoni mwa wataalamu waliowezeswa.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Kitalu nyumba Bw.Balabala Pundungu ambaye ni Afisa Kilimo Msaidizi aliyeteuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya. Aidha, Kitalu nyumba hiki kina ukubwa wa eneo lenye upana wa mita 8 na urefu wa mita 30 zenye ujanzo wa miche 780 aina ya “Kibo Star “ yenye uwezo wa kuzalisha kwa kila mche mmoja kilo 10 hadi 11 baada ya kuanza kuvuna mzao ya nyaya .
Wataalamu wengine wa Kilimo ni Catherine Hagile ambaye yeye ni mbobezi wa kilimo katika masuala ya mbogamboga na matunda (Horticulture) , Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kiteto Bw. Rodrick Kidenya ambaye husimamia kazi za Afisa Vijana Wilaya kwa kufuatilia mahudhurio ya vijana hawa na mhimili wa shuguli hii ni Bw. Christopher M. Simwimba ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa ujumla wao hawa ndiyo husimamia shughuli zote za mradi huu wa Kitalu nyumba.
Hata hivyo hii ni fursa pekee kwa vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya kiteto kutumia ujuzi huu ili kujiongeza kivingine namna ya kupata mtaji ili kuzalisha kibiashara kwa mtu moja mmoja, familia au kivikundi. Pia ni ajira kwa kuwa na elimu ya uzalishaji mazao haya kupitia teknolojia ya kitalu nyumba hivyo wamepanua wigo wa kufanya kazi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya kiteto na nje pia kwa ajili ya kujiletea maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.
Mwisho, tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, kwa kuleta mradi huu mkubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwani umefungua fursa lukuki kwa vijana, na sisi kama Halmashauri ya Wilaya tutahakikisha tunausimamia ipasavyo kadri iwezekanavyo ili matunda ya teknolojia hii yaendelee kwa vijana wengine wa wilaya hii.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa