Aprili 25,2025 Kamati ya Fedha,Uratibu na Mipango, kilifanya kikao cha Robo ya Tatu ya 2024/2025 katika eneo la Hifadhi za WMA Makame kwenye moja ya vitalu ambacho kinatumika kwaajili ya Utalii wa Uwindaji wilayani hapa.
Katika kikao hicho wajumbe waliipongeza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani hapa. Aidha wataalamu waliaswa kuzingatia matumizi sahihi ya fedha na kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati.
Pamoja na hayo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Abdallah Bundala, aliwapongeza wananchi kwa utunzaji na uhifadhi wa mazingira ambao umewezesha kupatikana kwa hifadhi hiyo ambayo imeleta wawekezaji.
Aidha alitoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira kwani hifadhi hiyo inaipatia halmashauri fedha ambazo pia zinatumika kutekeleza miradi mbalimbali wilayani hapa.
Vilevile alimshukuru Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki kwaajili ya wawekezaji nchini.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa