Kampuni ya Project CLEAR kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, imeendesha kampeni ya afya wilayani Kiteto ijulikanayo kwa jina la "Mtu ni Afya" mnamo Februari 2-3, 2025.
Kampeni hiyo imelenga kuwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya uchafu wa mazingira, ukosefu wa matumizi ya vyoo, lishe duni, na kutofanya mazoezi.
Uzinduzi wa kampeni ulifanyika katika kata ya Kibaya, ukiongozwa na balozi wa kampeni hiyo, msanii wa kugani mashairi Mrisho Mpoto. Akitoa elimu katika kampeni hiyo, msanii huyo aliwaasa wananchi kuweka mazingira safi, kunawa mikono kwa usahihi, kula mlo bora, na kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.
Kampeni hiyo pia iliambatana na mchezo wa mpira wa miguu kati ya mashabiki wa Simba na Yanga pamoja na mashindano ya maswali na majibu kuhusu elimu iliyotolewa. Washindi walizawadiwa pesa taslimu, vikombe vyenye nembo ya Mtu ni Afya, mipira, na tisheti.
Wananchi wa Kiteto waliojitokeza katika kampeni hiyo ambayo ilifanyia Kibaya, Matui na Engusero, waliahidi kutumia maarifa waliyopata kuboresha afya zao na mazingira wanayoishi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa