Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mh. Queen Cuthbert Sendiga, amewaagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani Kiteto kuhakisha wanaboresha barabara zote wilayani hapo ili ziweze kupitika vizuri haswa katika kipindi hiki ambacho wilaya inatarajia kupata mvua za kutosha.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo Novemba 15, 2023, kwenye ziara yake ya siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani hapo.
Akiwa wilayani hapo, Mh. Sendiga alikagua miradi ya barabara ikiwemo barabara ya Ngipa kuelekea Ndirigishi na barabara ya Engusero kuelekea Kiperesa ambapo barabara hizo kwa sasa zinafanyiwa maboresho yakiwemo ujengaji wa mitaro na madaraja.
Mh Sendiga alimuagiza Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Kiteto, Mhandisi Edwin Magiri, kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo kwa ufanisi ili iweze kukamilika kwa wakati ili wananchi wasipate tabu ya kutumia barabara hizo pamoja na nyingine zote ndani ya wilaya hiyo haswa katika kipindi hiki ambacho wilaya inategemea kupata mvua nyingi kama ambavyo imetabiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA).
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa