Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Makongoro Nyerere leo tarehe 1 June, 2021 amepongeza halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa kupata
hati safi katika taarifa ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka 2019/2020.
Mhe. Makongoro ameyasema hayo wakati akizungumza na baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto kuhusu
taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali akisema, majukumu ya mkuu wa mkoa yapo kwa mujibu wa sheria
Na. 19 ya mwaka 1997 kifungu cha 5 na kifungu kidogo cha (1) (2)
"Mkuu wa mkoa atakuwa na shughuli zote za serikali katika mkoa wake na kusimamia shughuli zote za msingi, kama vile ulinzi,
usalama na kusimamia sera za serikali za kisekta, kusimamia shughuli za utekelezaji wa maendeleo, kusimamia rasilimali fedha
na watu katika mkoa husika".
Alisema ziara yake kwenye kikao cha baraza hilo maalumu la madiwani ni kuzungumzia taarifa ya ukaguzi kama ilivyowasilishwa
na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, kwa mwaka 2019/2020 akisema ukaguzi haumanishi kutafuta makosa bali ni
njia ya kubaini mapungufu na kushauri namna ya kuondokana ama kutojirudia kwa mapungufu hayo na kuleta ufanisi katika usimamizi
wa rasilimali za umma.
"Mhe. Mwenyekiti nimesoma taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali pamoja na maoni yake kuhusu usimamizi wa
hesabu kwa halmashauri yako kwa mwkaa 2019/2020, nichukue nafasi hii kukupongeza wewe mwenyewe na baraza lako pamoja na
wataalamu kwa kupata hati safi kwa miaka mitau mfululizo kuanzia 2017/2018, 2018/2019 na 2019/2020 hongereni sana"
Alisema kupata hati safi ni matokeo ya usimamizi mzuri uliofanywa na baraza lako, kamati za kudumu za halmashauri na menejimenti
hongereni sana... kwa kupata hati safi, akisema pamoja na kupata hati safi ya ukaguzi baraza lako la madiwani lisimamie kikamilifu
manejimenti ya halmashauri yako.
Mweka Hazina wa wilaya ya Kiteto, Bi. Hadija Bofu akiwasilisha taarifa ya ukaguzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri
ya wilaya ya Kiteto Bw. Tamim Kambona alisema hoja nane za miaka ya nyuma zimefungwa na kusalia hoja tano ambazo zipo katika hatua
mbalimbali za utekelezaji
Alisema kati ya hoja 52 za mwaka 2019/2020, kati ya hizo 47 zimefanyiwa kazi na kufungwa, na hii ni kutoka na jitihada zilizofanywa
na menejimenti kwa kushirikiana na kamati za kisekta hali iliyofanya halmashauri ya wilaya ya Kiteto kupata hati safi kwa mwaka 2019/2020.
kwa upande wake Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Manyara Bw. Kenedy Kaganda ameeleza kuwa mkoa wa Manyara ni miongoni mwa mikoa
inayofanya vizuri katika taarifa za ukaguzi wa hesabu za serikali kutokana na kuwepo kwa mpango na mikakati ya kujibu hoja hizo huku
akisisitiza kuwa Wilaya ya Kiteto ambayo imejitahidi kuwa na hoja chache iendelee kupunguza na zibaki hoja za kisera tu,
Nao baadhi ya madiwani baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto akiwepo Mhe. Paul Tunyoni na Hassan Benzi wamemuomba
mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kufuta hoja za miaka ya nyuma na ambazo halmashauri hazina uwezo wa kuzifuta kwa kuwa
ni madeni ya vyama vya ushirika AMCOS ambayo hayalipiki, huku Mhe. Mbunge wa Jimbo la Kiteto Wakili Edward Ole Lekaita akishauri kuwa
kesi zilizopo mahakamani kati ya halmashauri na mzabuni sheria ichukue mkondo wake.
Akizungumzia hali ya usalama, Mkuu wa wilaya ya Kiteto Kanali Patrick Songea, alisema hali ni shwari ingawa kuna changamoto za
mipaka katika hifadhi ya Mkungunero iliyopo wilayani Kondoa na vijiji vya wilaya ya kiteto akidai jitihada zinaendelea kutatafuta
ufumbuzi wake ingawa aliomba mkuuwa mkoa kuingilia kati katika jitihada hizo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa