• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC Mnyeti Atangaza Kiyama kwa Wavamizi wa Misitu Wilayani Kiteto

Imetumwa : January 18th, 2018


                                                 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Lembapuli kata ya Lorela Wilayani Kiteto


RC Mnyeti Atangaza Kiama kwa Wavamizi wa Misitu Kiteto.


Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexanda Mnyeti amewataka wananchi  kuacha mara moja tabia ya kuvamia misitu na kukata miti kwa kisingizio cha mashamba.Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Lembapuri kata ya Lorela wilayani Kiteto katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Lembapuri  baada ya kuona uharibifu mkubwa   alipotembelea  msitu huo  uliopo katika kijiji hicho kuona maeneo yanayotambulika na wananchi wa wilaya ya Kilindi  na  wilaya ya Kiteto kuwa ni  mipaka kati ya wilaya hizo mbili  kwa mujibu wa GN namba 65 ya mwaka 1961 na GN namba 185 ya mwaka 1980.


 Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Mnyeti  amesema kwamba uharibifu wa misitu ni mkubwa sana, na  inapaswa kuchukua hatua za haraka kukomesha  uharibifu huo.Akisisitiza kuhusu kuchukuliwa hatua kali kwa wananchi wanaovamia misitu,Mhe. Mnyeti anasema ‘‘ mtu anapotaka kuvamia misitu  chukueni hatua. OCD  kamata watu wote waliovamia msitu wachukulie hatua za kisheria. Afisa misitu pitia maeneo yote yaliyovamiwa hesabu miti yote iliyokatwa ,wahusika  wote wakisha malizana na polisi wapande miti .Na ukumbuke kwamba ni miti kumi kwa kila mti mmoja uliokatwa. Wapande miti hiyo  chini ya uangalizi wa serikali”.


Katika hatua nyingine  wakazi wa kijiji hicho wamewasilisha  kero zao kwa mkuu wa mkoa ,ambapo kero kubwa  ni wavamizi kutoka kijiji cha Mafisa Wilaya ya Kilindi, uvamizi ambao umedumu kwa miaka takribani kumi sasa, ambapo wavamizi hao wamekuwa wakisababisha   uvunjifu wa Amani , Mauaji ,uharibifu wa mali,na uharibifu wa miundo mbinu ya maji .Kero nyingine ni  kunyang’anywa mashamba  yao yaliyopo katika kijiji cha Amei na kupewa watu wengine. Katika kushughulikia kero hiyo Mhe. Mnyeti  Aliwataka wanakijiji hao  hao kuwasilisha  nyaraka zao halisi zinazoonyesha umiliki wa mashamba hayo kwa mkuu wa wilaya ili aweze kutatua mgogoro huo.Hapa Mhe. Mnyeti anasema “ Mkuu wa wilaya shughulikia tatizo hili  la uvamizi wa Mashamba.Fukuza wote waliovamia mahamba ambayo sio ya kwao,waondoke maja moja.Ndani ya wiki moja wawe wameondoka ”.


Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Tumaini Maggessa amemueleza Mhe. Mnyeti sababu ya kuendelea kwa mgogoro huo ambapo amesema kwamba watu wa Kilindi na Kiteto wanagombania mpaka, na kwamba watu wa Kilindi waliingia katika eneo linalosadikika kuwa  ni eneo la Kiteto wakalifyeka wakatangaza kwamba  ndio mpaka kati ya Kilindi na Kiteto jambo ambalo wananchi wa Kiteto hawakubaliani nalo. Vilevile Mhe. Magessa ametoa ushauri wa jinsi ya kumaliza mgogoro huo .Mhe. Magessa anasema ‘‘ Nashauri kwamba GN namba 185  ya  mwaka 1980 ifutwe, na GN namba 65 ya mwaka 1961 ndiyo ifuatwe kuondoa huu  utata uliopo sasa”.Akijibu kuhusu mgogoro huo wa Kilindi na Kiteto  Mhe. Mnyeti amesema kwamba suala la  mgogoro wa mipaka kati ya kilindi na Kiteto litashughulikiwa kikamilifu na litakwisha, na  kwamba  watakutana na waziri wa ardhi , viongozi wengine pamoja na wataalamu wa ardhi  kujadili namna ya kumaliza mgogoro huo.


GN ni tangazo la serikali namba linaloainisha  mipaka.Tangazo la serikali ndilo linaloeleza  kwamba eneo fulani linaanzia wapi na kuishia wapi,iwe ni mkoa, wilaya ,tarafa, kata au kijiji. GN namba 185 ya mwaka 1980 na GN namba 65 ya mwaka 1961 ni matangazo ya serikali yanayoeleza mipaka kati ya Kilindi na Kiteto.


Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa