Mkuu wa Mkoa Wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akikabidhi mipira kwa timu za vijana wilayani Kiteto.Tukio lililofanyika Ikulu ndogo Kibaya Kiteto.
................ HABARI KAMILI......
RC Mnyeti Adhamiria Kukuza Soka Mkoani Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Axander Mnyeti ameahidi kuanzisha timu ya mpira wa miguu ya mkoa wa Manyara.Mhe. Mnyeti ameyasema hayo wakati akikabidhi mipira kwa timu za vijana. Ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa katika ziara zake wilayani Kiteto .
Akizungumza wakati akikabidhi mipira hiyo Ikulu ndogo ya Kiteto, Mhe. Mnyeti anasemaā€¯ leo nawakabidhi mipira hii kama nilivyokua nimeahidi.Mipira hii ni kwa ajili ya mazoezi,baaye nitatoa jezi na vifaa vingine. Na nitafanya hivi kwa wilaya zote za mkoa wa Manyara.Baada ya hapo nitaandaa mashindano ya pamoja, mtacheza,nitaleta wataalamu watachambua wachezaji wazuri, hatimaye tutapata timu ya mkoa wa Manyara,timu hiyo haitakuwa na upande wowote,itakuwa ni ya mkoa mzima . Tutaomba kucheza na timu kutoka nje ya mkoa , wachezaji watakaa kambini na tutacheza . Nataka baadae tuwe na timu ya mkoa,timu ambayo itashiriki mashindano mbalimbali ya kitaifa.
Sambamba na kukabidhi mipira hiyo Mheshimiwa Mnyeti ametoa angalizo kwa vijana kwamba ,anataka wacheze kwa sababu michezo ni afya, michezo ni ajira,ni umoja na ni amani, lakini wasicheze wakati huu wa msimu wa kilimo badala yake waende shamba .Baada ya kilimo ndipo watoke wacheze ili aweze kutekeleza ahadi ya kutafuta wachezaji wazuri kutoka katika timu hizo ndogondogo zilizopo wilayani hapa.
............. MWISHO ..............
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa