• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC Mnyeti Ampongeza DED Kiteto

Imetumwa : January 10th, 2018


Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti  akitoa pongezi  na maelekezo  kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona na kaimu Mhandisi wa ujenzi wilaya Mhandisi Chogo Mang'era  baada ya kukagua ujenzi wa uzio wa hospitali ya wilaya  ya Kiteto wakati alipotembelea hospitalini hapo.


                                                            Uzio wa Hospitali ya wilaya ya  Kiteto ambao ujenzi wake unaendelea ni moja wapo ya miradi ya maendeleo ambayo inasimamiwa na Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa ufanisi mkubwa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti  pamoja na ujumbe wake  wakiwasili katika  jengo la idara ya wagonjwa wa nje (OPD) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto



                                  Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto.Aliyesimama upande wake wa kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti  pamoja na ujumbe wake  wakiingia katika  wodi ya wanaume  wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto

                                                   

Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti akiwa ndani ya wodi ya wanawake   akipokea maelezo kuhusu upatikanaji wa vifaa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Kiteto  Dkt. Malkiadi Mbota  wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto



Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti  akiwa ndani ya jengo la upasuaji akipokea maelezo kuhusu uhaba wa wataalamu wanaoshughulika na  upasuaji  kutoka kwa Mganga Mkuu wa  wilaya ya Kiteto  Dkt. Malkiadi Mbota wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Kiteto.


Watumishi katika jengo la upasuaji hospitali ya wilaya ya Kiteto wakiwa tayari kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Alexander Mnyeti   akiwa ndani ya jengo la kitengo cha dawa na vifaa tiba  hospitali ya wilaya ya Kiteto akitoa maelekezo kuhusu udhibiti wa dawa  wakati alipotembelea hospitalini hapo.




                                                                                                                            ....... HABARI KAMILI........

RC MNYETI AMPONGEZA DED KITETO

Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti amempongeza Mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo .Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa uzio wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto alipotembelea hospitalini hapo mapema wiki hii.

Akizungumza wakati wa kukagua uzio huo mheshimiwa Mnyeti anasema ‘‘mkurugenzi kazi yako ni nzuri ,ukuta huu kujengwa kwa shilingi milioni 32 ni matokeo ya usimamizi mzuri. Nashauri miradi yote mtakayoendelea kuitekeleza itumie force account ili thamani ya fedha ionekane, nimependa sana kazi hii, kazi nzuri sana, pesa iliyotumika kidogo’’.

Akiwa hospitalini hapo mheshimiwa Mnyeti pia amemtaka mganga mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DMO) daktari Malkiadi Paschal Mbota kuhakikisha kwamba hakuna dawa inayo potea. Akisisitiza kuhusu udhibiti wa dawa mheshimiwa Mnyeti anasema ‘‘Mheshimiwa mkuu wa wilaya hakikisha dawa zinadhibitiwa . DMO sisi tuna wataalamu wetu wanatupa taarifa , tukibaini kwamba umeshindwa kusimamia madaktari wako , dawa zinapotea ovyo ovyo tutakuondoa''.

Aidha   mheshimiwa Mnyeti amemuagiza  daktari Mbota  kuhakikisha kwamba dawa zinapotolewa hospitali ya wilaya kwenda katika vituo vya afya, kamati za dawa katika vituo vya afya zipokee dawa,na zinapopokea zidhibiti matumizi ya dawa katika vituo hivyo ili dawa ziwafikie wananchi. Pia amemuagiza DMO  kutoa semina za mara kwa mara  juu ya umuhimu wa kudhibiti dawa kwa kamati za dawa na watumishi wanaohusika  na utoaji dawa .Vilevile mheshimiwa Mnyeti amewataka watumishi wa kitengo cha dawa na vifaa tiba kudhibiti upotevu wa dawa  ili kuongeza tija katika utumishi wao.

Katika ziara hiyo mheshimiwa Mnyeti alitembembelea maeneo mbalimbali ya hospitali  ikiwemo kitengo cha madawa na vifaa tiba, jengo la upasuaji , wodi ya wanaume ,wodi ya wanawake  pamoja na jengo la  idara ya wagonjwa wa nje (OPD), ambapo amewapongeza madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo  kwa kazi wanayofanya kuokoa maisha ya watu, na kuwatia moyo kwamba kazi wanayofanya ni kazi ya wito , waendelee kuongeza bidii kuwatumikia wananchi katika wito huo.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa