Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti Akihoji Kuhusu Utoro wa Wanafunzi Katika Shule ya Sekondari Kijungu Wilayani Kiteto Alipotembelea Shuleni hapo .
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kijungu Wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Alexander Mnyeti Alipotembelea Katika Shule Hiyo.
.......HABARI KAMILI ......
RC MNYETI ATOA AAGIZA KUKAMATWA KWA WAZAZI WA WANAFUNZI WATORO
Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti ameagiza kukamatwa kwa wazazi wa wanafunzi watoro. Mheshimiwa Mnyeti ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule ya sekondari Kijungu iliyopo katika kata ya Kijungu wilayani Kiteto na kuona mahudhurio mabaya ya wanafunzi katika shule hiyo .
Akiwa shuleni hapo Mhe Mnyeti aliagiza kuonana na wanafunzi , na baada ya wanafunzi kujipanga ,Mhe. Mnyeti alitaka kufahamu idadi kamili ya wanafunzi katika shule hiyo kwa kila kidato ,kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ,ambapo alielezwa idadi yao, idadi hiyo ilimsababisha Mhe. Mnyeti kutaka kufahamu pia na idadi ya wanafunzi walikuwepo shuleni kwa wakati huo, alipewa idadi yao, idadi ambayo ilimsukuma kutoa agizo kwa mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe.Tumaini Magessa , Mhe. Mnyeti anasema “ Hali ya mahudhurio katika shule hii ni mbaya sana .Walimu wapo shule,lakini wanafunzi hawapo.DC waite viongozi wa kijiji hiki mpange jinsi mtakavyoshughulikia utoro wa wanafunzi” .
Sambamba na kumuagiza Mhe. Tumaini Magessa kushughulikia tatizo hilo ,Mhe. Mnyeti pia amemuagiza Mkuu wa polisi wilaya ya Kiteto SP Fadhili Luoga kutoa askari polisi 4 ili washirikiane na mtendaji wa kijiji cha Kijungu katika kukamata wazaziwa wafunzi hao.Vilevile amemuagiza mkuu wa shule hiyo kuandaa orodha ya wanafunzi watoro na kuikabidhi kwa mtendaji wa kijiji kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.
......... MWISHO..........
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa