• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

RC Mnyeti Kuwashughulikia Wachochezi wa Migogoro Kiteto

Imetumwa : January 8th, 2018


                         Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti  Akisikiliza  Kero  Mbalimbali Zilizokuwa Zikiwasilishwa  Wakati  wa  Kikao Chake na Watumishi wa Serikali,Wenyeviti wa Vijiji Pamoja na Wahe. Madiwani  kilichofanyika ndani ya ukumbi wa Kituo cha Jamii (Community Center) Kibaya -  Kiteto

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa  Akiwasilisha Taarifa ya Wilaya  kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti Katika  Kikao cha Mhe.  Mkuu wa Mkoa na Watumishi wa Serikali,Wenyeviti wa Vijiji Pamoja na Wahe. Madiwani .




Watumishi wa Serikali,Wenyeviti wa Vijiji ,Wahe. Madiwani  pamoja na Kamati ya siasa ya wilaya ya Kiteto  wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti  ndani ya Ukumbi wa Kituo cha Jamii ( Community Center) Kibaya - Kiteto.


RC MNYETI KUWASHUGHULIKIA WACHOCHEZI WA MIGOGORO KITETO

Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti ameahidi kuwachukulia hatua watu wote wanaochochea migogoro wilayani Kiteto. Mheshimiwa Mnyeti ameyasema hayo katika kikao chake  na watumishi wa serikali,wenyeviti wa vijiji pamoja na waheshimiwa madiwani kilichofanyika ndani ya ukumbi wa kituo cha jamii (Community Center) kilichopo katika mji mdogo wa Kibaya .

Akizungumza katika kikao hicho mheshimiwa Mnyeti amesema kwamba iko migogoro ya ardhi inayoendelea wilayani Kiteto, kazi kubwa imefanywa na watangulizi waliotangulia katika  kushughulikia migogoro hiyo, mkuu wa wilaya aliyeko sasa amefanya kazi kubwa kupunguza migogoro hiyo, na kwamba imefika wakati sasa migogoro hiyo ifike mwisho. Kadhalika mheshimiwa Mnyeti  amesema kuwa migogoro ya Kiteto ina sura nyingi, kwani  ipo migogoro  ambayo ni ya muda mrefu sana,ipo migogoro yenye mantiki ,lakini pia ipo migogoro isiyo na  mantiki ambayo inasababishwa na wanasiasa na   watu wengine  ambao wanaichochea migogoro hiyo kwa faida zao binafsi,

Aidha mheshimiwa Mnyeti amekemea vikali tabia ya baadhi ya watu  kufufua na kuendeleza migogoro ambayo ilishatatuliwa, ambapo amewataka kuacha mara moja tabia hiyo, na hapa   mheshimiwa Mnyeti  anasema‘‘Migogoro ya Kiteto imewachosha watu, hatuwezi kuwa tunaendekezana, tunavumiliana kumbe yuko mtu ambaye  kwa migogoro hii yeye ananufaika . Anachochea migogoro halafu anakaa pembeni anasubiri bomu lilipuke DC ukimbizane. Jana nimesikia sentensi moja mtu anasema bora sasa Rais alete DC mwingine tuwe na maDC  wawili, mmoja awe kazi yake ni kushugulikia migogoro, na mwingine wa kutafuta  maendeleo ya Kiteto. Serikali  haiwezi kufanya biashara ya namna hiyo, nitawachulia hatua’’. Pia  amewataka wakazi wa Kiteto kufahamu kwamba maelekezo yote ya serikali wilayani yanatolewa na mkuu wa wilaya .Mkuu wa wilaya ndiye mtu wa mwisho,maelekezo yake ndio sahihi na ndio ya mwisho,hivyo mtu mwingine yeyote haruhusiwi kutoa maagizo juu ya maagizo ya mkuu wa wilaya.
 
 Mheshimiwa Mnyeti pia amewataka watumishi wa serikali kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, kwani kumekuwepo na vitendo vya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya watumishi, hususani tabia ya ulevi uliokithiri na watumishi kutofika katika vituo vyao vya kazi. Vitendo ambavyo vinasababisha wananchi kulalamika kwa kukosa huduma.

Katika hatua nyingine mheshimiwa Mnyeti amezungumzia suala la elimu, ambapo amesema kwamba mkoa wa Manyara  ni wa mwisho katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba.Kutokana na hali hiyo, Mheshimiwa mnyeti   ametengua uteuzi wa waratibu elimu kata pamoja na walimu wakuu wa shule zote ambazo hazikufikia ufaulu wa asilimia hamsini(50%) katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa mwaka 2017. Vilevile amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim Kambona  kuhakikisha kwamba shule zote zinakuwa na uwiano sawa wa walimu, na kwamba uhamisho uanze mara moja kuhamisha walimu kutoka katika shule zenye walimu wengi, hususani shule zilizoko maeneo ya mijini na kuwapeleka katika shule zenye walimu wachache ambazo ziko vijijini. Sambamba na hilo mheshimiwa Mnyeti  amempongeza mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magessa kwa hatua anazochukua katika kupambana na tatizo la mimba mashuleni na amemtaka kuongeza  jitihada zaidi ili kuondoa tatizo hilo.






Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MAFUNZO YA MFUMO WA E-UTENDAJI KWA WATUMISHI.

    June 12, 2025
  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa